Naibu waziri wa Uchukuzi, Enjinia Dk Athuman Mfutakamba (Mbunge) akimkabidhi bendera Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel tayari kuiwakilisha nchi katika mashindano ya urembo wa Dunia (Miss World 2011) yaliyopangwa kufanyika London, Uingereza Novemba 6.
Mbali ya kukabidhi bendera, Naibu Waziri pia alimchangia salha Dola 1000 kwa ajili ya safari hiyo huku wafanyakazi wa wizara yake wakitoa Shs Milioni 3.4.Pia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kilikabidhi Dola 2000 mrembo huyo kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Nakuala Senzia.
Senzia pia alimkabidhi Salha kifurushi kinachoelezea vivutio vya utalii na uwekezaji vya Tanzania ambavyo Salha atavitumia wakati wa kuinadi nchi akiwa kambini na mashindano hayo. Picha na Maelezo kwa Hisani ya kitengo cha Habari cha Miss Tanzania.
No comments:
Post a Comment