Thursday, October 27, 2011

Waliofariki kwenye ajali ya basi la deluxe wazikwa kibaha leo

Majeneza yaliyo beba mabaki ya miili yawatu walio kufa kwa kuteketea kwa moto baada ya basi la Deluxe lililokuwa likitokea Dar kuelekea Dodoma kupata ajali na kuwaka moto katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani juzi,yakiwa yamepangwa tayari kwa ibada ya pamoja mchana wa leo
Majeneza yakiendelea kupangwa kwa ajili ya ibada ya pamoja.
Baadi ya Viongozi wa dini wakiwa katika ibada ya kuwaombea marehemu waliofariki kwenye ajali ya Basi la Deluxe iliyotokea Kibaha,mkoani Pwani juzi.
Taratibu za mazishi zikiendelea kwenye makaburi hayo.
Viongozi wa dini wakijumuika pamoja na waombolezaji wengine katika shughuli ya kuihifadhi miili ya ndugu zetu waliofariki kwenye ajali ya basi la Deluxe iliyotokea Wilayani Kibaha juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mh. Mwantumu Mahiza akilia kwa huzuni wakati shughuli za Mazishi zikiendelea.
Sehemu ya waombolezaji waliojumuika katika mazishi ya ndugu zetu waliofariki kwenye ajali ya basi la Deluxe juzi..
Picha na Chris Mfinanga wa Globu ya Jamii,Pwani
Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

No comments: