Sunday, October 9, 2011

Wanafunzi wa Kiafrika washutumiwa kwa biashara ya Ukahaba Malaysia, wamo wa Kitanzania pia

Pichani ni Baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa nje ya club kusibiri wateja, Huko Jalan P-Ramlee jijini Kuala Lumpur Malaysia.

Na Pius Micky.

Imeripotiwa kuwa baadhi ya wasichana wa kiafrika wengi wao wanaokwenda nchini Malaysia kwa njia ya masomo ya juu wamejiingiza kwenye biashara ya ukahaba.

Kwa mujibu wa gazeti kubwa la nchini Malaysia The Star, wanafunzi hao wamekuwa wakionekana hadharani nje ya kumbi za starehe/burudani hasa nyakati za usiku huku wakionekana wakizungumza na wateja wao kwa kupatana bei.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,wakinadada hao ambao wanachaji kiasi cha RM 200 kwa show time (chap chap) sawa na Tsh 80,000/- na RM 600 ambayo ni sawa na laki tatu kasoro ushee kwa kulala hadi asubuhi.

Nchi ya Malaysia imekuwa kimbilio kwa wanawake wengi wanaojiuza toka nchi nyingi hasa za jirani na Malaysia kwa vile jiji la Kuala Lumpur limekuwa likipokea watalii wengi hasa wanaokimbia majira ya baridi huko nchi za Ulaya.

Kwa miaka ya karibuni kumekuwa na wanafunzi wengi sana toka nchi za Afrika wakienda kusoma nchini Malaysia kutokana na elimu yao kuwa ya kiwango cha juu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanafunzi hao ambao wana umri kati ya miaka 20 hadi 30 inasemekana wanatoka nchi za Ghana, Tanzania, Togo, Cameroon, Botswana na Nigeria.

Kwa mujibu wa ripoti za kichunguzi toka jarida la Star Metro linasema wana dadapoa hao wana uwezo mkubwa wa kumkamata mteja kutokana na vigezo wanavyovitumia ambavyo vina mshawishi mteja kwa haraka.

Wanafunzi hawa wote huwa wanakuwa na copy za Passport zao pamoja na barua zinazoawatambulisha kuwa ni wanafunzi toka vyuoni mwao.

“Niko hapa kwa miezi miwili tu na utafurahia huduma yangu” alisema mmoja wa mabinti hao mwenye umri wa miaka 22 ambaye alijitambulisha kuwa yeye ni Binti wa Kitanzania.

Kumekuwa na wimbi kubwa la wanafunzi wa Kiafrika kwenda kusoma Malaysia, na kiumweli kuna tatizo kubwa sana ambalo wanakutana nalo wanafunzi hao wakiwa huko Malaysia,kwani hairuhusu kwa wanafunzi yeyote wa kigeni kufanya kazi na hata ukipata kazi ya kufanya huwa hazilipi kama ilivyo kwa nchi zingine.

Mdau Pius Micky ambaye alishoka kwenye nchi hiyo ya Malaysia aliiambia Globu ya Jamii kuwa hali hiyo ipo na kwa wanafunzi hao na anaongea kutokana na Experience alinayo na mji ule.

Maisha nchini Malaysia ni magumu hasa kama huna kipato na unategemea kupata pesa toka kwa wazazi kwani ukikosea hesabu inabidi ukae mpaka pesa zitumwe tena toka nyumbani,hali ambayo inawapelekea wanafunzi wengine kuingia katika biashara hiyo.

Jijini Kuala Lumpur maisha yako juu kulinganisha na miji mingine nje ya jiji hilo, wengi wa wanafunzi ni kweli wamekuwa wakifanya biashara hizi na wengine wamejiingiza kwenye biashara hatari ya madawa ya kulevya ambayo haina adhabu mbadala nchini Malaysia/ Singapore zaidi ya kunyongwa ndani ya masaa 24.

Tunawaasa wazazi wa watoto hao wawe karibu na watoto wao na wajue gharama halisi za kusomesha watoto nchini humo ambazo ma agent wengi wa shule hawawaambii ukweli wazazi kuhusu gharama hizi, matokeo yake wakifika kule ndio wanatumbukia humo.

No comments: