Saturday, October 1, 2011

WANAWAKE 220 WAJIFUNGULIA KATIKA KITANDA KIMOJA HUKO LOISINONI



NA GLADINES MUSHI ARUSHA





Zaidi ya wazazi 220 kutoka katika kijiji cha Losinoni katika Halmashauri ya Arusha vijijini wanalazimika kujifungulia katika kitanda kimoja kwa kila mwaka kwa kuwa zahanati ya kijiji hicho haina vitanda kwa ajili ya wodi ya kujifungulia (labour ward) hali ambayo inawalazimu baadhi ya wazazi kujifungulia nyumbani, huku wengine wanaokwenda hospitalini hapo kulazimika kujifungulia chini.


Hayo yamebainishwa na mganga mfawadhi wa zahanati hiyo Bw Salumu Abdalah wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mapema jana katika kijiji cha Losinoni ndani ya halmashauri ya wilaya ya Arusha vijijini.


Aidha Bw Abdlah alieleza kuwa hali hiyo inatokea kwa kuwa mpaka sasa zahanati hiyo ambayo inaweza kuwahudumia wanawake wajawazito pamoja na watoto imekuwa na kitanda kimoja hali ambayo inazua madhara makubwa sana kwa wajawazito hao


Alendelea kueleza kuwa mpaka sasa kuna madhara mbalimbali ambayo yameonekana kutokea sana mara baada ya zahanati hiyo ambayo inyomilikiwa na serikali kukosa vitanda na vifaa maalumu kwa ajili ya kujifungulia wanawake.


"Hii hali ya kuweza kuzalisha wanawake zaidi ya 200 kwenye kitanda kimoja kweli ni mbaya sana kwa kuwa baadhi ya wanawake ambao wanakuja hapa kujifungua au kuweza kuona wazazi wanashindwa kupata hamu ya kuweza kujifungulia hospitalini kwa kuwa hamna vitanda vya kutosha hali ambayo inafanya hata idadi ya wanaojifungulia majumbani kuongezeka kwa wingi"alisema Bw Abdalah


Hataivyo aliongeza kutokana na hali hiyo ambayo inakabili zahanati hiyo kwa sasa wanawake ambao wanajifungua wanalazimika kulala chini kwa kukosa vitanda hali ambayo nayo ina madhara makubwa sana kwa wanawake hao ambao wanajifungua.


'Hapa kwa kweli wanawake wanapata sana shida kwa kuwa wanapokuja zaidi ya wanawake wawili hasa nyakati za kujifungua inabidi kwanza mmoja wao aweze kulala chini yaani ajifungulie mtoto akiwa sakafuni na mwingine kitandani hali ambayo ina madhara makubwa sana kwa wanawake hao.


Aliendelea kwa kusema kuwa ni vema kwa sasa serikali ikahakikisha kuwa inajiwekea utaratibu maalmu wa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii hususani huduma za afya kwa kuwa hali hiyo inazaa matunda makubwa sana kwa wanawake hao ambao hawana uwezo maalumu wa kwenda katika vituo vikubwa vya afya .


Nao wanawake wa eneo la Losinoni walisema kuwa ni vema kama wakadumishiwa zaidi huduma za afya kwa kuwa wanapokosa huduma za afya hasa za uzazi salama wanaongeza idadi ya wanawake wanaojifungulia zaidi majumbani badala ya mahospitalini.

No comments: