Saturday, October 1, 2011

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII YAZINDUA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda akitoa hotuba ya kuzindua rasmi wiki ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ambapo pamoja na mambo mengine ameelezea vipaumbele vitakavyozingatiwa baada ya miaka 50 ya Uhuru kuwa ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii, Kuimarisha huduma za Afya ya Wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wenye umri chini ya miaka 5 ikiwa ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoammbikiza na yasiyoambukiza pamoja na yale yaliyosahaulika.Pia ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupima Bure Afya zao na kipindi chote cha wiki ya maadhimisho hayo itakayomalizika tarehe 2, Oktoba, 2011.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Rufaro Chatora akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo ameipongeza Tanzania kwa hatua iliyofikia katika kuboresha huduma ya Afya.
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Deo Mtasiwa akitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kusheherekea miaka 50 ya Uhuru.
Mwanamuziki Mkongwe nchini Kassim Mapili (katikati) akiwa na wanamuziki wenzake wa bendi ya Mjomba wakitoa burudani katika sherehe za maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Mh Dkt. Mponda akisakata Rhumba baada ya kukunwa na muziki uliokuwa ukiporomoshwa na Mzee Kassim Mapili.
Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Mlandwe Madihi (mwenye miwani) akimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Dkt.Mponda alipotembelea banda la Taasisi hiyo.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wakurugenzi, Viongozi wa Wizara na Serikali, Wadau wa Sekta ya Afya na Watoa huduma za Afya.

No comments: