Tuesday, October 11, 2011

Watanzania Wanaosoma nchini Korea ya Kusini waomba kuwepo kwa ubalozi nchini humo

Spika Makinda (katikati) akiwa na Bw Emmanuel Lupil ambaye ni Mwenyekiti( Kulia0 na Bw. Severini Kapinga Katibu wa Watanzania waishio Korea.
Bw. Lwenje akifafanua jambo.
Kipindi cha maswali na ufafanuzi.
Mtanzania aishiye Korea Kusini mtoto Faith Sanga akitoa zawadi kwa Mhe. Spika kwa niaba ya kundi zima.
Mwendesha shughuli Bi Juliana Masawe akimpongeza Faith na kumshukuru Mhe. Spika kwab kuja kuonana nao.
Picha ya pamoja.Picha zote na Prosper Minja-Bunge.

Wakati wa kuahirisha ziara yake nchini Korea Kusini jana jioni, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda alikutana na watanzaia wanaoishi nchini humo katika Chuo Cha Maendeleo cha Korea (KDI) ambapo waliiomba serikali kupitia kwake (Spika) kutafakari kufungua ubalozi nchini Korea Kusini kwani kuna mengi yatakayoinufaisha Tanzania. Tayari nchi jirani ya Kenya imefungua ubalozi nchini Korea.

Watanzania hao wapatao sitini ambao wengi wao ni wanafunzi wa elimu ya juu walitanabaisha kuwa Korea Kusini ni nchi ambayo ilikuwa maskini sana miaka michache iliyopita lakini imefanya mapinduzi ya kiuchumi na sasa ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea duniani.

“Ni bora kujifunza kutoka kwenye nchi zinazokuwa kwa kasi tukiziona kuliko kutegemea nchi zilizoendelea zamani kama vile za ulaya na Marekani” alisema Bw. Lwenje ambaye ni mwanafunzi wa shada ya uzamili ya uchumi.

Katika risala yao, wameiomba serikali pia itumie vizuri fursa za masomo zilizopo nchini Korea kwa kupeleka wanafunzi wengi zaidi kwa manufaa ya nchi. Aidha waliiomba serika iharakishe mpango wa kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwani ni jambo ambalo kwa sasa hivi halikwepeki tena.

Mhe. Spika akiwaahidi kuyafikisha maombi yao serikalini amewataka kudumisha nidhamu, kufanyakazi kwa bidii na kudumisha uzalendo wa nchi yao.

“Ninyi ndiyo chachu na wakala wa mageuzi mara mtakapomaliza masomo yenu na kurejea nyumbani mkiwa na utaalamu na uzoefu wa yale mtakayokuwa mmejifunza huku” aliwaasa Mhe. Makinda.

Aliwahamisha kuwa hali ya numbani ni shwari ila changamoto ni nyingi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kwamba jitihada kubwa zinafanyika kuondoa tatizo la umeme na mchakato wa katiba mpya unaendelea.

No comments: