Friday, November 11, 2011

Ajali Mbaya ya Basi la Sumry na Gari dogo la Prado jana Mbele kidogo ta Hotell ya aljazila





Picha mbalimbali za ajali mbaya iliyotokea jana katika sehemu ya Mtandika, mbele kidogo ya hoteli maarafufu ya Al Jazeera, mkoani Iringa, iliyohusisha basi la Sumry na gari aina ya Prado iliyokuwa ikiendeshwa na daktari bingwa wa macho katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya. Katika ajali hiyo daktari huyo alifariki papo hapo (kama inayoonekana katika picha), Na katika basi hakuna aliyepoteza maisha licha ya majeraha madogo madogo. Dereva wa basi alikimbia baada ya ajali hiyo na hivi sasa anatafutwa na jeshi la polisi. Chanzo cha ajali ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi alikuwa akijaribu kulipita lori (ku-overtake) katika kona na kukutana uso kwa uso na gari hiyo ya Prado ambayo pia ilikuwa kasi sana.
Imeletwa na mdau ambaye ni muhanga wa ajali hiyo

No comments: