Rais waZanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali MohamedShein,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ua kuwasili katikauwanja wa ndege wa kimataifa was Abeid Amani Karume Air Port,akitokeanchi za UAE,katika ziara za kuimarisha uhusiano wa kihistoria na nchihizo. Picha na Othman Maulid Habari naMaelezo Zanzibar
Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kufukia eneo la Bahari kwa lengola kuongeza Ardhi kwa ajili ya makaazi ili kupunguza ujenzi katikamaeneo ya kilimo.
Hayoyameelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DkAli Mohammed Shein wakatia akizungumza na Waandishi wa Habari hapoUwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar mara baadaya kurejea ziara yake katika nchi za Falme za kiarabu
AmesemaSharjah imeshafanya kazi hiyo kwa ufanisi na kufanikiwa kujenga nyumbaza makaazi katika maeneo ambayo yalikuwa ya bahari hapo awali.
Aidhaamesema Nchi kama Uholanzi na nyigi nyenginezo zimeshafukia bahari nakujengwa miji ya kisasa kabisa bila ya tatizo lolote.
Hivyoalisema Zanzibar inayo maeneo ambayo yakifukiwa yataweza kujengwanyumba nyingi za maendeleo kwani miaka ya nyuma kazi hiyo ilifanywakatika maeneo ya Funguni hadi Makumbusho ambalo eneo lote hilo lilikuwaBahari.
Akizungumziasuala Uwekezaji Dk Shein alisema wakati umefika kwa Zanzibar kupatamaendeleo ya haraka kwa kukaribisha wawekezaji wa uhakika katika Nyanjambali mbali ili kuweza kuongeza pato la taifa.
Amesemakuwa katika mazungumzo yake na viongozi wa Sharjah na Ras Al khaimawameonyesh hamu ya kuendeleza maeneo hayo ili yaweze kuchangia katikauchumi wa Zanzibar.
Kuhususuala la Maji safi na salama amesema Serikali ya Sharjah italetawataalaam wa kuangalia vianzio vipya vya maji kwani utafiti uliofanywaumeonyesha kwamba maji katika visiwa vya Zanzibar yamepungua hivyo ipohaja ya kutafuta vianzio vipya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Akizungumziajuu ya mafunzo kwa vijana wa Zanzibar Dk. Shein amesema kuwa Sharjah naRas Al khaima wamekubali kuwapokea vijana wa zanzibar katika Vyuo vyaombalimbali ikiwemo masomo ya Udaktari.
AmewaombaViongozi wa Chuo kikuu cha Sharjah kuja Zanzibar kutembelea Chuo Kikuucha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona nyanja gani za mafunzo ambazowataweza kushirikiana.
No comments:
Post a Comment