Thursday, November 17, 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AFUNGUA MDAHALO WA NAFASI YA UMUHIMU WA KATIBA KATIKA MAISHA YA WATANZANIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo Novemba 17, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika jumba hilo na kuangalia baadhi ya picha za matukio zilizowekwa katika jumba hilo kama kumbukumbu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma moja ya kitabu kilochokuwa katika meza ya maonyesho ya vitabu katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, baada ya kufungua rasmi Mdahalo wa wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania, uliofunguliwa leo Novemba 17, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika maonyesho ya Jumba la Makumbusho ya Taifa kuangalia picha za baadhi ya Mashujaa wa Harakati za ukombozi zilizowekwa katika jumba hilo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim na (kulia) ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Salim Ahmed Salim (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku (wa pili kushoto) wakati akiiwasili kwenye Jumba la Makumbusho ya Taifa leo Novemba 17 kwa ajili ya kufungua Mdahalo wa Nafasi ya Umuhimu wa Katiba katika Maisha ya Watanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa katika mdahalo huo kutoka Unguja.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais



No comments: