Thursday, November 24, 2011

The Foundation for Civil Society yatoa tuzo kwa asasi za kiraia zilizofanya vizuri 2011

Pichani ni Asasi ya Saidia Wazee Karagwe ikishangilia vilivyo mara baada kujinyakulia tuzo ya ushindi wa jumla katika tuzo hizo


Mgeni rasmi pichani shoto,Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika yasiyo na Kiserikali,Bw.Narsil Katemba akimkabidhi tuzo mwanaharakati Mama Marry Lusimbi ambaye ametoa mchango mkubwa wa ushawishi na utetezi wa kuongeza idadi ya uwakilishi wa usawa Kijinsia katika vyombo vya maamuzi.


Pichani shoto ni Mbunge wa Viti Maalum,Mh Devotha Likokola akishangilia pamoja na kundi la Belita Group mara baada kuwakabidhi tuzo yao mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya utoaji tuzo kwa asasi za kiraia zilizofanya vizuri 2011,kundi hilo limeibuka na tuzo hiyo ikiwa ni moja ya kundi lililofanikiwa katika suala zima la uwezeshaji kwa akina mama/wanawake.
Mgeni rasmi,Mkurugenzi wa Idara ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Bw.Narsil katemba akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia utoaji tuzo kwa asasi za kiraia zilizofanya vizuri 2011,tuzo hizo zilikuwa zikitolewa na The Foundation for Civil Society sambamba na mbia mwenza Oiko Credit.



Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society,Bw. John Ulanga akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasiku kubwa,ndani ya moja ya ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl,Ubungo Plaza jijini Dar.


Sehemu ya meza kuu ikifuatilia jambo kwa umakini,lililokuwa likiendelea jukwaani
Wageni waalikwa wakijadiliana jambo kwa pamoja
Burudani pia ilitolewa na kundi la Akanashe Group kama uonavyo pichani.
Wageni waalikwa wakifuatilia jambo kwa makni.
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo
Mrisho Mpoto na kundi lake wakitumbuiza kwenye hafla hiyo.

********************

The Foundation for Civil Society/ Oiko Credit zatoa tuzo kwa
asasi za kiraia zilizofanya vizuri 2011.
Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for Civil Society, John Ulanga amesema utaratibu wa kutoa tuzo kwa asasi za kiraia zinazofanya vizuri zaidi katika utekelezaji miradi yao umechochea uwajibikaji na utendaji kwa asasi nyingi,amesema kuwa taasisi hiyo inatoa ruzuku kwa asasi zaidi ya 300,lakini kuna asasi 700,Aidha Ulanga ameongeza kuwa wanatoa tuzo hizo pia kuzithamini asasi zile zinazofanya vyema zaidi,na kwamba ili wengine wajifunze kwa wnegine.

Bw. Ulanga alibainisha hayo hapo jana jioni jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuzizawadia asasi za kiraia (CSO Excellence Awards 2011), zilizofanya vizuri kwa utekelezaji wa miradi yao anuai kwa jamii, hafla iliyoandaliwa na taasisi hiyo ya kijamii,aidha Ulanga alisema utaratibu huo wa kuzikumbuka kwa tuzo asasi na wanaharakati waliochangia shughuli hizo ulioanza kutekelezwa mwaka 2008, umeleta mabadiliko makubwa hasa ufanisi katika utekelezaji wa miradi kutokana na ushindani uliokuwa ukijitokeza miongoni mwa asasi hizo.

Alisema miongoni mwa vipengele vilivyozingatiwa katika utoaji wa zawadi hizo ni pamoja na Ushiriki Sera, Utawala Bora, Uwajibikaji na Asasi iliyojenga uwezo na Ukuzaji wa Mitandao. Asasi mbalimbali zilizofanya vizuri zaidi zimejinyakulia zawadi katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo na wanaharakati wa masuala ya kijamii. Asasi ya Saidia Wazee Karagwe imetwaa ushindi wa jumla katika tuzo hizo.

No comments: