Thursday, November 24, 2011

KUTOKA IRINGA.....MADUKA YAVUNJWA IRINGA USIKU WA LEO


Wananchi wakitazama Stationery ya Nyigi iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso ambayo imevunjwa na wezi


Mmiliki wa duka la Ferick Urembo akiangua kilio kwa uchungu baada ya kukuta duka lake limevunjwa na kuibwa mali mbali mbali asubuhi hii.

Wananchi wa Manispaa ya Iringa wakitazama duka la Ferick Urembo ambalo limevunjwa usiku wa leo .
NA FRANCIS GODWIN
Wakati maandalizi ya sikuu kuu za Krismas na mwaka mpya yakianza taratibu ,watu wanaosadikika kuwa ni wezi nao wameanza kufanya maandalizi ya funga mwaka baada ya usiku wa leo kuvunja maduka mawili eneo la Eso katika Manispaa ya Iringa na kuiba mali mbali mbali.

Maduka ambayo yamevunja usiku wa leo ni pamoja na duka la Ferick Urembo lililopo eneo la Natioanl katika majengo ya Bakwata , na Nyigu Stationery iliyopo eneo la jengo la Masiti Eso.

Baadhi ya wamiliki wa maduka hayo wamesema kuwa maeneo yao yamekuwa yakilindwa na makampuni ya ulinzi na hadi sasa eneo la tukio walinzi wa wamu hawapo.

Katika duka la Ferick Urembo watu hao wanaosadika kuwa ni wezi wamechukua mali mbali mbali ukiwemo urembo vyote vikikisiwa kufikia kiasi cha TS.milioni zaidi ya 2 huku katika Stationery ya Nyigu kompyuta na mali mbali mbali zimechukuliwa na ambavyo vyote thamani yake bado kufahamika .

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umefika eneo la tukio na kushudia vilio vikiwa vimetawala kwa wamiliki wa maduka hayo tukio ambalo bado limekusanya umati mkubwa wa watu

No comments: