Wednesday, November 30, 2011

HATIMAE BARABARA YA ARUSHA KARATU YAANZA KUPITIKA JAPO KWA TARATIBU

Hatimaye mawasliano ya barabara kati ya Arusha na Karatu yamerejea kama mwanzo baada ya barabara hiyo kushindikana kupitika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisa kufurika kwa mto kirurumo ambao ulimwaga maji mengi hivyo kusukuma mawe na magogo na kupelekea kuziba barabara pamoja na kusababisha mtu mmoja kupoteza maisha.hivi sasa magari yanapita ng'ambo na watembea kwa miguu pamoja nawatalii ambao walikuwa wakienda katika hifadhi ya ngorongoro.
Baadhi ya Mifugo ikipita upande mmoja wa barabara huku upande mwingine ukiwa umesheheni mawe.
Picha na Chris Mfinanga.

No comments: