Wednesday, November 16, 2011

Kada Wa CCM Auwawa Iringa

WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa silaha wamemuua kwa kumpiga risasi mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Kisanga kata ya pawanga wilaya ya Iringa vijijini jimbo la Ismani mkoani Iringa Abeid Mhuvila ambaye ni kada wa Chama cha mapinduzi (CCM)
Mashuhuda wa tukio hilo wamemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa watu hao walitenda mauwaji hayo majira ya saa 3 usiku wa kuamkia leo na kuwa walifika katika kijiji hicho wakidai wapo katika msako wa kutafuta punda wao ambao walidai wamepotea.
Hata hivyo baada ya kufika nyumbani kwa mwenyekiti huyo walimkuta akiwa nje ya nyumba yake pamoja na familia yake na kueleza shida yao na baada ya hapo waliomba kuonyeshwa mwenyekiti huyo .
Afisa mtendaji wa kata hiyo ya Pawaga Jumanne Lusigi akithibitisha kutokea kwa mauwaji hayo alisema kuwa taarifa za kuuwawa kwa mwenyekiti huyo zilianza kujulikana usiku na kuwa wananchi walilazimika kufanya msako bila mafanikio .
Alisema kuwa baada ya mauwaji hayo wauwaji hawakuweza kuchukua kitu chochote kutoka katika nyumba ya marehemu huyo wala kufanya unyama wa aina yeyote kwa familia yake.
Diwani wa kata ya Ilolo Mpya Fundi Mihayo akielezea tukio hilo alisema kuwa ni tukio la kinyama na kuwa bado limeacha maswali mengi zaidi kwa wananchi wa wilaya nzima ya Iringa kutokana na mazingira ya mauwaji hayo ambapo wauwaji hawajachukua mali yoyote wale fedha.
Mbunge wa jimbo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) akizungumzia mauwaji haya kwa njia ya siku alisema kuwa taarifa ya kuuwawa kwa mwenyekiti huyo aliipata juzi usiku na kulazimika kutoa taarifa polisi .
Hata hivyo mbali ya kutoa pole kwa familia ya marehemu Mhuvi kwa kumpoteza ndugu yao bado alisema kifo hicho ni pengo kubwa kwa wananchi wa kijiji cha Kisanga ,kata ya Pawaga na jimbo zima la Isimani na kuwa mchango mkubwa wa kiutendaji wa mwenyekiti huyo ni pengo kubwa kwa Taifa.
Na Francis Godwin - Iringa

No comments: