Friday, November 4, 2011

MGANGA WA JADI AMLAWITI MTEJA WAKE MTOTO WA MIAKA 12


NA FRANCIS GODWIN

Mwanamke aliyefariki dunia baada ya Kubikiriwa na Kulawitiwa na Mume Wake(picha ya maktaba)
MTOTO wa miaka 12 mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amefanyiwa ukatili ikiwa pamoja na kulawitiwa baada ya kupelekwa kwa mganga wa jadi kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa kuanguika.

Mwandishi wa mtandao huu Oriver Moto anaripoti kuwa akielezea mkasa huo mama wa mtoto ( jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) alisema alimpeleka kwa mganga wa jadi baada ya kijana wake kupata matibabu baada ya kuona ugonjwa huo wa kuanguka unamsumbua.

“Nilikuwa ninahangaika na mwanangu, nikaona nijaribu na dawa za kienyeji labda atapona, na nilipomfikisha kwa mganga mama Adelina Mgomela nilimuacha huko ili akamilishe dozi, lakini mtoto alikuwa anakimbia anarudi hapa nyumbani, mimi namrudisha tena kwa mganga, kumbe mwanangu alinificha alikuwa anafanyiwa uchafu, na Dr. Kidasi” Alisema mama huyo.

Alisema mtoto huyo amekaa huko kwa zaidi ya miezi 4 na kila akitoroka akimkuta nyumbani mtoto anamchapa na kumuamuru kurudi nyumbani kwa mganga.

Alisema kuna siku mtoto alimwambia kuwa anakimbia kwa mganga kutokana na mjomba wake ambaye ni mtoto wa mganga Mgomela anamfinya mgongoni na ndipo aliamua kwenda nyumbani kwa mganga huyo ili kumueleza juu ya mkasa anaofanyiwa mtoto wake, na pia alimuomba mganga huyo kulala na mtoto wake.

“Sikujua kama alikuwa anamfanyia unyama huo mwanangu, aliponambia kuwa mjomba wake anamfinya usiku nilikwenda nyumbani kwa mama Semgomela nikamueleza mateso anayoyapata mwanangu, na nikamuoma awe analala nae chumbani kwake, lakini juzi aliporudi nikaona mtoto amebadilika kama anaumwa, na lilitambua kuwa hayupo vizuri baada ya kutoka chooni, kwani alikuwa hana furaha, nikahisi kunakitu kinamsibu,” Alisema.

Alisema baada ya kumuuliza mtoto huyo alimueleza kitendo alichokuwa akifanyiwa nyumbani kwa mganga aliyemtaja kwa jina la Dr. Kidasi.

“Niliishiwa nguvu niliposikia maneno hayo, nikamuuliza mwanangu sasa kwa nini hukunieleza haya yote tangu siku ile uliporudi hapa nyumbani kwa mara ya kwanza??, Akasema Dr. Kidasi alimwambia akinieleza atamuua kwa kumkata na panga,” Alisema mama wa mtoto.

Naye mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema mtoto wa mganga huyo Dr. Kidasi alikuwa akimfanyia ukatili huo kila siku usiku kwa madai kuwa hiyo ndiyo dawa iliyomfanya mama yake ampeleke hapo.

“Alisema ni dawa itakayonisaidia nisianguke, ndiyo maana na mama nikienda nyumbani ananirudisha ili nimalize dawa, na alikuwa ananiambia kuwa nikimueleza mtu dawa anayonipa atanikata na panga na nitakuwa siendi kuokota mikusu ( Matunda ya asili ya polini), “ Alisema mtoto huyo.

Hata hivyo uongozi wa serikali ya kijiji ulipofika eneo hilo la tukio uliamuru mama huyo kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Ifunda ili mtoto aweze kupatiwa matibabu Hospitali.

Huku mgambo wa kijiji Julius Mitao aliamuru kundi linguine kufika nyumbani kwa mganga huyo ili kumtia nguvuni Dr. Kidasi na baada ya kufika nyumbani kwa mganga zoezi hilo liligonga mwamba kwani mtuhumiwa hakuwepo kwa madai ya kuwa ametoka kwenda kuchukua hela.

Lakini baadhi ya wananchi walisema mama huyo baada ya kupata taarifa za mtoto wake kufanyiwa kitendo hicho alikubalina na mganga huyo kulipwa shilingi elfu hamsini, ili kumaliza mgogolo huo, na baada ya mganga kushindwa kutimiza makubaliano ya kulipa kiwango hicho cha fedha ndipo aliamua kuwaeleza wenzie wakazi wa kijiji hicho kwani hakukuwa na hatua zozote zilizochukuliwa juu ya mtuhumiwa pamoja na mtoto huyo kupatiwa matibabu.

No comments: