Friday, November 4, 2011

MH NYALANDU ATEMBELEA KIWANDA CHA PANASONIC, AWAPONGEZA KWA BIDHAA ZENYE UBORA.

Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada(Kushoto), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Katikati) na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako( Kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda cha Panasonic.


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (Kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako(Kushoto) mara baada ya kuwasili katika kiwanda hicho kwa ziara fupi. Katikati ni Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada.
Kutoka kushoto. Balozi wa Japan hapa nchini Bw Masaki Okada, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Patrick Marwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini TBS Bw Charles Ikelege( Kulia) akielezea ubora wa bidhaa za kampuni ya Panasonic ambayo ni miongoni mwa kampuni za mwanzo kabisa kupata nembo ya Ubora kutoka TBS.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu (kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja Mkuu wa kiwanda cha Betri cha Panasonic Bw Yoshiyuki Sako (katikati) kuhusu ubora wa betri zinazozalishwa na kiwanda cha Panasonic cha jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Patrick Marwa.

No comments: