Friday, November 4, 2011

TACAIDS yakutana na waandaa watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza

Mtoa mada kutoka TACAIDS Grory Mziray akitoa mada katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza jana.
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza,Goddfrey Mabu Chambuko akichangia mada katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watangazji na wandaaji wa vipindi vya redio za kijamii kutoka mikoa ya kanda ya ziwa.
Afisa Uhusiano wa TACAIDS, Grory Mziray akisoma moja ya malengo ya washiriki wa mafunzo ya kuwajerngea uwezo waandaaji wa vipindi na watangazaji wa redio za kijamii yanofanyika jijini Mwanza.
Richard Ngaiza akitoa mada ya nguvu ya redio za jamii katika kuleta mabadiliko kwa jamii kuhusiana na maambukizi ya VVU kwa washiriki.
washiriki wa mafunzo ya kujengewa uwezo wakimsikiliza mtoa mada,Richard Ngaiza wa kampuni ya Masoko AGENCIES (T) LTD kuhusu nguvu ya redio za kijamii

Na Mashaka Baltazar, MWANZA

TUME yaTaifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imendaa mafunzo ya siku kuwajengea uwezo watangazaji,waandaaji na watayarishaji wa vipindi vya redio za kijamiii wa mikoa ya Kanda wa Ziwa, kupitia mtaalamu elekezi,Kampuni ya Masoko ANGENCIES (T) Ltd.

Mafunzo hayo yana lengo la kukuza uelewa kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi (HIV/AIDS) kwa jamii, kuboresha vipindi vinavyohusiana na Ukimwi na kuharakisha na kuchochea zoezi la kubadili tabia katika jamii.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika jijini Mwanza yakishirikisha waandaaji wa vipindi na watangazaji wa redio za kijamii, wapatao 80 kutoka katika mikoa yaMwanza, Kagera,, Mara na Shinyanga.

Akitoa mkakati wa mafunzo hayo Afisa Uhusiano wa TACAIDS, Grory Mziray alisema mafunzo hayo kwa watangazaji na waandaji wa vipindi watawezesha kuharakisha kampeni ya mbalimbali na malengo tarajiwa dhidi ya mapambano ya ukimwi kwa vile vituo vinasikika zaidi katika jamii zinazowazunguka.

“TACAIDS wameona vema kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo watangazaji na waandaaji wa vipindi vya redio za kijamii, kote nchini ili kukuza uelewa, afya kuhusiana na ukimwi na kuelimisha jamii ili iweze kubadili tabia kwa kutumia vipindi mbalimba vitakavyoandaliwa na kutangazwa kupitia vituo vya redio hizo za kijamii” alisema Mziray

Mbali na hilo waandaaji na watangazaji watafundishwa stadi za namna bora za kuandaa ama kutengeza vipindi bora vya ukimwi ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu,katika kuimareisha utendaji wa TACAIDS.

Alisema redio hizo zitatumika kutoa taarifa sahihi kwa jamii ili iweze kuelewa athari za ukimwi na kufahamu umuhimu wa kupima ili kujua afya zao, na kuweza kujitambua na kujua namna ya kuishi kwa ambao wameambukizwa VVU.

Wananchi waishio katika maeneo mengi ya mjini wako katika hatari kubwa ya kuambukizwaVVU kuliko vijijini , ingawa vijini wanawake wanaathirika kutokana na maumbile.

Changamoto nyingine ni kwa wanawake kujiingiza katika biashara ya ngono kwa ajili ya kipato, ngono kinyume cha maumbile na kuwa na wapenzi zaidi ya wawili, ambapo matumizi ya kondomu yako chini kwa kiwango cha wanawake 22 na wanaume 34 wanaoweza kutumia mipira kujikinga na mambukizi.

Mada mbili zilitolewa katika mafunzo hayo ambazo ni hali ya ukimwi nchini iliyotolewa na Grory Mziray wa TACAIDS na nguvu ya redio jamii katika kuleta mabadiliko ya maambukizi ya VVU iliyotolewa na Richard Ngaiza kutoka kampuni ya ANGENCIES (T)Ltd.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu walioambukizwa na wanaishi na VVU inafikia milioni 1.5 ambapo mkoa wa Iringa ukiwa unaongoza Kwamba tatizo la kutopima ni moja ya changamoto kubwa zinazokabili jamii na TACAIDS katika udhibiti wa maambukizi mapya ya VVU.

No comments: