Friday, November 11, 2011

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC)Atembelea Makaburi ya wataalam wa Kichina Na Kufanya Mazungumzo na Ujumbe wa Chama Cha Cha Mapinduzi(CCM)Nakukutana na Rais Jakaya Kikwete

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akiweka shada la maua kwenye eneo la Makaburi ya wataalam wa Kichina alipokwenda kuyaona, eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam.
UJUMBE wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, ukipata maelezo ulipotembelea Kampuni ya Reli ya TAZARA
Rais Jakaya Kikwete akimkaribisha Ikulu, Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho. Katikati ni Msekwa. Rais Kikwete akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, Ikulu Dar es Salaam, leo.
Kutoka Kushoto Msekwa, Wilson Mukama na baadhi ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa wakiwa kwenye mazungumzo hayo.
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho, akimpa zawadi Makamu Mwenyekiti wa CCM Pius Msekwa baada ya mazungumzo ya ujumbe wa Chama hicho na Ujumbe wa CCM katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kimomunisti cha China (CPC) Liu Yunshan ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya chama hicho na Mwenyeji wake Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM baada ya mazungumzo ya ujumbe wake na wa CCM kuwa na mazungumzo katika ukumbi wa sekretarieti, Ofisi Ndogo yab Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba Dar es Salaam. Wengine ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape NNauye, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama na Katibu wa NEC, Uhusiano wa Kimataifa Januari Makamba.
Picha na Bashir Nkromo


No comments: