Moto huo ulianza kuwaka toka majira ya saa 9 Alasiri hadi majira ya saa 3 usiku bado jitihada za kuuthibiti ilionekana kugonga mwamba baada ya kusambaa zaidi na kuingia maeneo ambayo gari la zimamoto kutoka Manispaa ya Iringa kushindwa kuingia porini zaidi kutokana na kukosekana barabara.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa chanzo cha moto huo kichaa bado kufahamika japo umechomwa na mtu asiyefahamika.
Huku mkuu wa shule ya sekondari St Mary's Ulete Joseph Kibiki akisema kuwa jitihada za kuzima moto huo eneo la shule ziliweza kuzaa matunda japo uwezekano wa kuzima moto huo katika maeneo yanayozunguka shule hiyo yalionyesha kugonga mwamba.
Alisema kuwa baada ya kuona moto huo ni mkubwa zaidi walilazimika kupiga simu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini ili kuomba msaada wa gari la zima moto ambalo limeonyesha kuwa msaada mkubwa katika kuzima moto huo kwenye maeneo jirani na makazi ya watu.
Mkuu huyo alisema kuwa bado hajatambua usalama wa wanafunzi ambao waliingia porini kuzima moto huo kwani hadi majira ya saa 3 za usiku walikuwa hawaja rejea bwenini kutoka kuzima moto huo.
No comments:
Post a Comment