Friday, November 4, 2011

MOTO WATEKETEZA MALI ZA SHULE YA KANISA ST MARY'S SEKONDARI ULETE


Mkazi wa ulete katika wilaya ya Iringa vijijini akizima moto mkubwa uliokuwa ukiteketeza mali za shule ya sekondari St Mary's Ulete ,shule inayomilikiwa na kanisa na Romani katoliki (RC)jimbo la Iringa


Wanafunzi wa shule ya sekondari St mary's Ulete wakitoka nje ya mabweni yao baada ya kuzingirwa kwa moto mkubwa


Masista wa kanisa la Roman Katoliki Ulete wakiwa na matawi la miti wakijipumzisha baada ya kuzima moto bila mafanikio


Wananchi wa ulete na wanafunzi wakitazama moto mkubwa ambao ulikuwa ukiendelea kuteketeza misitu mali ya shule ya sekondari St mary's


Moto ukiendelea kuteketeza mali mbali mbali ikiwemo misitu ya miti


Mzimu wa moto umeendelea kuteketeza mali za Makanisa baada ya asubuhi ya leo nyumba ya kanisa la Anglikana Dayosisi ya Iringa kuwaka moto eneo la Gangilonga mjini Iringa ,moto mkubwa ambao bado chanzo kufahamika umeteketeza mali mbali mbali ukiwemo msitu mali ya kanisa la Romani Katoliki (RC) jimbo la Iringa huku shule ya sekondari na wanafunzi wa shule hiyo ya St Mary's kunusurika .


Moto huo ulianza kuwaka toka majira ya saa 9 Alasiri hadi majira ya saa 3 usiku bado jitihada za kuuthibiti ilionekana kugonga mwamba baada ya kusambaa zaidi na kuingia maeneo ambayo gari la zimamoto kutoka Manispaa ya Iringa kushindwa kuingia porini zaidi kutokana na kukosekana barabara.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa chanzo cha moto huo kichaa bado kufahamika japo umechomwa na mtu asiyefahamika.

Huku mkuu wa shule ya sekondari St Mary's Ulete Joseph Kibiki akisema kuwa jitihada za kuzima moto huo eneo la shule ziliweza kuzaa matunda japo uwezekano wa kuzima moto huo katika maeneo yanayozunguka shule hiyo yalionyesha kugonga mwamba.

Alisema kuwa baada ya kuona moto huo ni mkubwa zaidi walilazimika kupiga simu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini ili kuomba msaada wa gari la zima moto ambalo limeonyesha kuwa msaada mkubwa katika kuzima moto huo kwenye maeneo jirani na makazi ya watu.

Mkuu huyo alisema kuwa bado hajatambua usalama wa wanafunzi ambao waliingia porini kuzima moto huo kwani hadi majira ya saa 3 za usiku walikuwa hawaja rejea bwenini kutoka kuzima moto huo.
Habari na picha kwa hisani ya Francis Godwin

No comments: