Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemiah Mchechu akisaini hati za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC,Lawrence Mafuru kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano kuhusu suala la mikopo ya nyumba jijini Da es Salaam leo, Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Injinia Kesogukewele Msita
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (kushoto) akishikana mikono na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru katika hafla ambayo Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lilisaini hati za makubaliano kuhusu mikopo ya nyumba na benki saba nchini. Benki hizo ni NBC, NMB, BOA, EXIM, Azania, KCB na CBA. Wa pili kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT) Lila Mkila na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka (katikati, nguo ya Pink), Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa benki saba zilizosaini makubaliano ya ushirikiano na NHC.
No comments:
Post a Comment