Mjumbe wa Mkoa vijana CCM-KILIMANJARO Bw Paul C. Makonda
--
Ndugu waandishi wa habari,kwanza napenda kuwashukuru sana kwa kuitikia wito huu kuja hapa leo.
Nianze kwa kuwapongeza kwa mara nyingine kwa juhudi zenu za dhati katika kuchochea mijadala muhimu ya Taifa letu na pia juhudi zenu mnazoendeleza za kufichua maovu mbalimbali bila uoga wowote mpaka htua ya kutishiwa maisha kwa baadhi yenu.Ni wazi kuwa vyombo vya habari katika taifa letu vimedhihirisha kuwa ni ni mhimili mkubwa wa demokrasia ya kweli.
Niko hapa kuelezea mambo machache ya msingi yanayoendelea katika taifa letu,ambayo bila kuwa na juhudi za dhati katika kuyatafutia majibu yake yanaweza kugeuka kuwa chanzo cha migogoro na migawanyiko itakayoathiri maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
Moja ni mijadala iliiyopamba moto inayowahusisha vijana wa makundi mawili ya Arusha na Pwani kuhusu wapi anatakiwa kutoka Rais ajaye.Mjadala huu umekuwa wa muda mrefu na umekuwa ukichukua sura mpya kila inapoitwa leo.Ni vizuri kukumbuka kuwa taasisi ya uraisi ni taasisI kubwa na inayoathiri hatima ya Taifa letu,hivyo kuacha mijadala inayohusisha ukanda katika kumpata Rais ajaye ni kuhatarisha amani na mshikamano uliodumu kwa muda mrefu.
Hapa ni kusema kuwa,mijadala hii itaendela kushika kasi kila siku zinapozidi kusogea.Hebu tujiulize kama leo,miaka 4 kabla ya uchaguzi mijadala hii inaanza kutugawa itakuwaje mwaka mmoja kabla ya uchaguzi?Na je ikitokea ameshinda wa kanda mojawapo inaonekana wazi wale wa kanda nyingine hawatamuunga mkono.Hii ni dalili ya dhahiri ya hatari kwa umoja ndani ya chama na nchi yenyewe.
Ni vyema nieleze kuwa,mgawanyo wa kikanda utaleta mpasuko mkubwa katika nchi kama hautashughulikjiwa mapema.Sababu ya msingi hapa ni kwamba watu watasahau dini zao,vyama vyao na wataanza kutukuza asili yao.Hatari kubwa itakayokuwepo mbeleni ni kuwa na Rais ambaye atakapokuwa madarakani bila woga atawapendelea walio wake.
Kama ili likiachiwa,ni wazi kuwa tutaona vijana wa kusini wakisimama na kuanza kudai Rais atoke kwao kabla ya kushuhudia vijana wa kanda ya ziwa nao wakiandamana kudai atoke upande wao.Hali ikifika hapo ni wazi kuwa nchi itakuwa katika mgawanyiko mkubwa.Ni vizuri tuiache demokrasia ya kweli inayohusisha vyama na sio ukanda ichukue nafasi yake.
Ni vizuri vijana hawa wanaokabiliwa na hali mbaya ya maisha,kukosa ajira na kutojua hatima yao wahusishwe katika mijadala ya kujikwamua kutoka katika hali zao ngumu badala ya kupoteza muda wa miaka 4 uliobaki kuendelea kuligawa Taifa kwa hoja ambazo haziwezi kuboresha maisha yao ya kila siku.
Maoni yangu katika hili ni kuona viongozi wajasiri na wanaoipenda nchi yao wakisimama na kulikemea kwa nguvu zote bila kuumauma maneno.
Plili,Kufuatiwa hoja hii,hivi karibuni kiongozi mmoja mwandamizi wa serikali ametoa tamko kuwa vijana waachiwe wajadili suala hili la Urais.Kwa nafasi yake nashawishika kuwa huu ulikuwa ni msimamo wa serikali juu ya jambo hili.
Napenda kutumia nafasi hii kusema kuwa msimamao huu ni vyema ukaangaliwa upya kwani hauna tija yoyote kwa Taifa na manufaa ya vijana kwa ujumla.Mjadala huu hautaweza kuleta ajira kwa vijana,hautarudisha matumaini kwa wanyonge,hautatengeneza ajira mpya wala hautatoa chakula kwa wale wanaoteseka na njaa.
Ni vyema sasa serikali ikachochea mijadala yenye manufaa na inayoonyesha kuathiri hatima ya vijana kuliko kuliko kuutia chachu mjadala huu.
Hoja za msingi kama vile:
vijana wananufaikaje na wawekezaji,mabilioni yaliyotolewa na Mh.Rais yamewanufaisha vipi vijana wa Tanzania,vijana wa vyuo vikuu watasaidiwaje na serikali ili wapate mikopo itakayowasaidia kumaliza masomo yao
Viana wa Tanzania wananufaikaje na fursa za soko la Afrika mashariki,na hata kuangalia kwa undani zaidi kwa nini serikali imeendelea kung’anga’nia kuilipa dowans huku nkukiwa kuna viongozi waandamizi wanaoonyesha wazi kupingana na maamuzi hayo.
Hzi ndizo hoja za msingi zinazotakiwa kupewa vipaumbele na viongozi wetu na si vinginevyo.Ningependa kuchukua fursa hii kuwasihi vijana wa Tanzania,tusikubali kutumika kuigawa Tanzania kwa Maslahi ya wachache wenye uchu wa kupata nafasi ya Urais 2015.Tutoe kipaumbele kwa mijadala itakayoleta majibu kamili ya matatizo yanayotukabili.Ni vyema tukumbuke maneno ya wenye hekima.”Waovu hustawai pale wema wanaponyamaza kimya”,ndio maana leo nieamua kusema.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Paul C. Makonda
No comments:
Post a Comment