LEO ASUBUHI MKOANI MWANZA KULITOKEA MAANDAMANO YA WAISLAM AMBAYO YALISABABISHA VURUGU KALI,AMBAPO WATU 19 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MPAKA SASA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA REBELATUS BARLOW AMESEMA KUWA BAADHI YA WATU HAO WAMEKAMATWA KATIKA ENEO LA MAHAKAMA YA WILAYA YA NYAMAGANA.
AMESEMA WANAOSHIKILIWA NI MIONGONI MWA WAFUASI WA DINI YA KIISLAMU WALIOFIKA LEO MAHAKAMANI HAPO KUFUATILIA KESI YA KUCHOMA KITABU KITUKUFU CHA DINI YA KIISLAM, QURANI.
KESI HIYO INAWAHUSU WATU WANNE WANAODAIWA KUCHOMA KITABU HICHO AMBAO WALIFIKISHWA MAHAKAMANI KUJIBU TUHUMA WALIZOKUWA WANAKABILIWA NAZO..
HAKIMU MKAZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NYAMAGANA, JANET MASESA AMEWAJA WATUHUMIWA HAO KUWA NI TUMAINI JUMANNE, PETRO MASHAURI, KALISTA MLOMO NA DIKSON MAGAI.
VURUGU HIZO ZILITOKEA BAADA YA HAKIMU HUYO KUAHIRISHA KESI HIYO HADI NOVEMBA 24 MWAKA HUU HATUA AMBAYO ILIPINGWA NA WAUMINI HAO.
No comments:
Post a Comment