Tuesday, November 15, 2011

VURUGU ZA WANANCHI IRINGA,ASKARI NA WAANDISHI WAJERUHIWA VIBAYA


Majeruhi wa mapingano kati ya polisi na wananchi mjini Iringa leo
Mwanahabari
wa kituo cha radio Overcomers Fm Devota Romanus akiwa wodi namba 7
katika Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kujeruhiwa mguu wake wa
kushoto kwa mawe
Askari polisi aliyejeruhiwa akipelekwa wodini kulazwa




Nguo za majeruhi ambaye alijeruhiwa kwa risasi baada ya kutaka kuwachoma moto wanahabari na polisi ndani ya nyumba hiyo




wananchi wakiwa nje ya lango la nyumba hiyo wakitaka kuonyeshwa watu wanaodaiwa kufa na kuonekana wakiwa hai (Misukule)Wananchi wakiishambulia nyumba yenye wanahabari na watuhumiwa na polisi kwa mawe.




Nyumba ya mfanyabiashara huyo ikiwa imevunjwa na wananchi


Habari Na Francis Godwin Iringa
Zaidi ya watu 10 wakiwemo askari wanne na wanahabari wamejeruhiwa
huku baadhi yao wakitibiwa na kuruhusiwa na wengine kulazwa katika
Hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuibuka kwa mapigano hayo kati ya
polisi na wananchi ,mapigano ambayo yametokana na imani potofu za
wananchi katika kuamini ushirikina.

Wananchi hao zaidi ya 200
walivamia nyumba ya mzee wa kanisa moja la kilokole katika mji wa
Iringa eneo la Frelimo jina limehifadhiwa kwa sababu za kimaadili .

Hata
hivyo pona ya wanahabari na polisi waliokuwa wamefungiwa ndani
ya nyumba hiyo na kushambuliwa kwa mawe na kunusurika kuteketezwa kwa
moto wakiwa ndani ya nyumba hiyo ilionekana baada ya askari polisi
wa FFU kutumia mbinu kubwa ya kulazimika kutumia risasi ya moto
kumshambulia mguuni mmoja kati ya watu wanaodaiwa kutaka kuongoza
wengine kuichoma moto nyumba hiyo iliyokuwa na wahahabari ndani
,polisi na mchungaji mmoja .

Baadhi ya wananchi wamelipongeza
jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa kuokoa maisha ya wanahabari hao na
watu wengine zaidi ya 10 ambao walipaswa kuuwawa na wananchi hao .

Wananchi
hao walionekana kuongezeka idadi baada ya FFU kuwatisha kwa mabomu
ya machozi huku wakidai kuwa mabomu hayo hayaui na bila polisi kupata
mbinu ya haraka ya kutumia risasi ya moto zaidi ya watu hao 10
wakiwemo wanahabari waliokuwa ndani ya nyumba hiyo wangekuwa
wameuwawa na wananchi hao ambao waliondoa imani na kikosi hicho kuwa
wamehusika kuificha misukule hiyo.

No comments: