Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kuhusu zoezi linaloendelea la uingizaji wa taarifa za sensa ya majaribio kwenye mfumo kwa komputya mara baada ya kumalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo.
Mtaalamu wa Kampuni ya DRS Gabriel Kago (katikati) akitoa ufafanuzi jana jijini Dar es salaam kwa waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa taarifa zilizopo katika dodoso la sensa la majaribio katika mfumo kwa komputya mara baada ya kumalizika hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini. Kulia ni Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo na kushoto ni Mtaalamu wa Mifumo ya Komputya (IT) wa NBS Mwanaidi Mahiza.
Mtaalamu wa Mifumo ya Komputya (IT) wa NBS Mwanaidi Mahiza akimwonyesha Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo (kushoto) akishuhudia zoezi hilo.
Kamisaa wa Sensa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Paul Kimiti(katikati) akielezea jijini Dar es salaam kuhusu jinisi sensa ya majaribio iliyomalizika hivi karibuni itawawezesha kuimarisha maandalizi ya sensa hapo mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa (kushoto) akiwa na Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo wakiangalia dodoso katika NBS jana jijini Dar es salaam lililotumika katika sensa ya majaribio iliyomalizika hivi karibuni.
Mwakililishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu(UNFPA) DKt. Julitta Onabanjo(kulia) akiongea na waandishi wa habari kuhusu zoezi la uingizaji wa taarifa za sensa katika mfumo wa komputya mara baada ya kumalizika kwa sensa ya majaribio hivi karibuni. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina A. Chuwa (kushoto).
(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam).
No comments:
Post a Comment