Friday, December 2, 2011

Kamati ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Umma Yatinga Ubalozi Wa Washington,DC

Bw. Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania Washington DC akimkaribisha Ubalozini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia Hesabu za Umma Mhe. John Cheyo(Mb.) ambae amefuatana na Mhe. Betty Machangu(Mb. CCM Viti Maalum Kilimanjaro)ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Nje,Ulinzi na Usalama ya Bunge na Bw. Theonest Ruhibalake, Mkurugenzi wa Bunge. Mhe. Cheyo na ujumbe wake wapo Washington DC kutembelea majengo ya Serikali pamoja na kujionea wenyewe hali halisi ya majengo hayo.
Bw. Suleiman Saleh akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. John Cheyo,Mhe. Betty Machangu na Bw. Theonest Ruhibalake ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC.
Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akiwa na Mhe. John Cheyo na ujumbe wake mara baada ya kutembelea jengo la zamani la Ubalozi wa Tanzania Washington DC

No comments: