Friday, December 2, 2011

PRECISION AIR YAPANDA MITI 5000 KATIKA MAGEREZA MWANZA

Mkurugenzi wa Usafirishaji wa Mizigo wa Precision Air Bw. Elias Moshi akipanda mti wa kwanza katika magereza ya Butimba jijini Mwanza. Kampuni hiyo ikishirikiana na shirika la Mazingira na Uhifadhi Tanzania (TEMCO) imeweza kupanda jumla ya miti 5000 katika eneo hilo.
Mkuu wa Magereza ya Butimba Bw. Edson Yalimo akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkurugenzi wa Usafirishaji Mizigo wa Precision Air Bw. Moshi na Mwenyekiti wa TEMCO Bw. John Masweta.
Wafanyakazi wa shirika la ndege la Precision Air na TEMCO wakiwa katika picha ya pamoja na utawala na maaskari wa magereza ya Butimba jijini Mwanza.

Precision Air-shirika la ndege linaoongoza Tanzania ikishirikiana na Shirika la Mazingira na Uhifadhi Tanzania (TECO) kwa pamoja wameweza kupanda miti zaidi ya 5000 katika magereza ya Butimba leo jijini Mwanza kama namna ya kuinua uhifadhi wa mazingira nchini.

Mkurugenzi wa usafirishaji wa mizigo wa Precision Air Bw. Elias Moshi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, alisema kwamba wakati Tanzania ikisheherekea miaka 50 ya uhuru sasa, ni vyema tukawakumbuka na kuwaandalia mazingira bora watanzania wa vizazi vijavyo ili na wao waweze kufaidi matunda ya nchi yetu huko baadaye.

“Kupanda miti si jukumu la serikali tu bali ni kwa watanzania wote kwa ujumla. Ndo maana leo kama wafanyakazi wa Precision Air tumeamua kutoa kipaumbele katika mazingira ili kuwa mfano kwa wananchi wengine,” aliongeza.

Pia Bw. Moshi alipendekeza serikali kupitisha mpango maalumu wa kupanda miti na kukagua kama wamiliki mbali mbali wa ardhi wanafuata hiyo. Akisisitiza kwamba ungekuwa mpango madhubuti ya kuhifadhi mazingira nchini.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa TECO Bw. John Masweta alisema kwamba katika miaka 50 ya uhuru ya Tanzania ingependeza zaidi kama watu watasherehekea kukiwa na uhakika wa mazingira bora pia.

“Kusema tunashehereka miaka 50 ya uhuru tu peke yake haitoshi, bali ni vizuri tukatafakari kuhusu namna tunavyoathiri mazingira yetu na tunaweza kufanya nini ili kuweza kuyaboresha,” alisema.

Kwa pamoja Bw. Masweta na Mkurugenzi wa Precision Air Bw. Moshi waliishukuru utawala wa magereza ya Butimba kwa nafasi yakipekee waliyopewa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Magereza ya Butimba Bw. Edson Yalimo alisema ni jambo jema Precision Air walilofanya wakishirikiana na TECO kuyakumbuka hata mazingira ya watanzania waishio magerezani.

“Tunawashukuru sana kwa kujali kwenu alisema,”alisema.

No comments: