Monday, December 12, 2011

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye Akabidhi Matrekta Kwa Wakulima Kondoa

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akijaribu kuliendesha trekta kabla ya kukabidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Singida, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi matrekta mawili diwani wa Kata ya Kwadelo mkoani Singida, Omari Kariate, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Trekta hizo ambazo ni mkopo kutoka Shirika la SUMA JKT, ni kwa ajili ya wakulima wa Kata hiyo. Wengine pichani ni Wajumbe kutoka Chama Cha Wakulima wa Kata hiyo waliohudhuria makabidhuano hayo.Picha na Bashir Nkoromo
---
NA MWANDISHI WETU
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amewataka viongozi kuongoza kwa vitendo badala ya maneno.


Nape alisema hayo wakati akikaidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadeo wilaya ya Kondoa mkoni Singida, katika hafla iliyofanyika leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

Wakulima wamepata matrekta hayo kwa mkopo kutoka Shirika la Suma JKT, kupitia mpango wa kuhamasisha kilimo cha kisasa unaosimamiwa na diwani wa kata yao ya Kwadelo, Omari Kariate.


Wamefanikiwa kukokpeshwa matrekta baada ya kuweza kulipa asilimia 50 ya gharama yote ya ununuzi ambayo trekta moja ni sh. milioni 25.


"Ili mapinduzi ya kweli yaweze kufikiwa katika kilimo na sekta nyingine za maendeleo ni lazima sasa viongozi waepuke mtindo wa kufanya kazi wa nadahria tu, badala yake wajikite katika kuonyesha vitendo, diwani huyu ameonyesha mfano mzuri wa kuingwa", alisema Nape.

Nape alisema hatua ya diwani huyo kuanzisha mpango na kuuhamasisha kwa wananchi hadi kukubalika na kuweza kutoa matunda si jambo la mzaha ni suala la dhamira ya kweli katika uongozi.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, diwani wa Kata hiyo, Kariate alisema, mpango wake wa kuhamasiaha wakulima kuwezeshwa kutumia matrekta umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa sasa kata hiyo ina jumla ya trekta tisa zote za mkopo kutoka SUMA JKT.

Alisema, kupitia mpango huo sasa wakulima wa kata hiyo wanaweza kulima kisasa zaidi na hivyo kujipatia mavuno mengi kuliko kutumia jembe la mkono. wilaya ya Kondoa hulima mazao ya mahindi, uwele na alizeti.



No comments: