Monday, December 12, 2011

Rais Wa Zanzibar Dk. Ali Shein Afungua Rasmi Kongamano la Mabadiliko Yan Tabia Nchi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akifungua kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel leo,lililotayarishwa na Chuo Kikuu cha taifa Zanzibar SUZA.
Mwakilishi wa Idara maalum inayoshuhulikia misaada kutoka Uingereza,DFID Angus Millers,akitoa hutuba yake wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel leo,lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,
Baadhi ya washiriki na wadau mbali mbali wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,katika ukumbi wa Zanzibar Ocean View Hotel leo,lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,wakifuatilia kwa makini mada zilizotolewa katika kongamano hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Prof Idrissa Ahmada Rai,Makamo Mkuu wa Chuo cha Taifa Suza,alipowasili katika viwanja vya Ocean View Hotel kulifungua kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi,katika ukumbi wa Mikutano Zanzibar Ocean View Hotel leo,lililotayarishwa na Chuo Kikuu cha taifa Zanzibar SUZA.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar












No comments: