Monday, December 5, 2011

KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU KUTANA NA MPIGANAJI WA VITA YA KAGERA ASIYEKUBARI MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA





Mzee
Cuf, akipozi kwa picha na kamera yake akiwa katika moja ya hafla za
Kitaifa miaka ya nyuma, (kulia) ni Mpiga picha wa Waziri Mkuu wa sasa,
Hirary Bujiku.






Mzee Cuf akiwa katika moja ya pori wakati akiwa katika Vita ya Kagera, kwa mujibu wa Mzee Cuf ilikuwa ni Agost 24, 1978.






Mzee Cuf (kulia) akiwa na mwenzake, wakiwa katika harakati za vita ya Kagera, 1978.









Salum
Ally ama ukipenda kwa jina maarufu kwa jijini Dar es Salaam na katika
baadhi ya mikoa ambayo hufanyia shughuli zake ni (Mzee Cuf), huyu yeye
ni Mpiga picha maarufu wa picha za kuuza al-maarufu kama Picha za
Manyaa.

Picha
za Banyaa ni zile picha zinazopigwa katika shughuli yeyote ikiwa ni
Mkutano ama sherehe bila mpigwaji kuwa na mkataba na mpigaji na kisha
huletewa picha ikiwa tayari na kuuziwa.

Mzee Cuf, kwa upande wake pamoja na
kuwa
ni maarufu zaidi katika fani ama ujuzi wa kupiga picha lakini yeye
amekuwa bado hadi hii leo haamini Kamera zinazoendana na mabadiliko ya
Teknolojia yaani kamera za 'Digital', kiasi kwamba hadi leo hii bado
anaamini kwa kufanya kazi na kamera yake aliyokwishaizoea ya Nikkon ya
kutumia Filim.


Akizungumza
na Mtandao wa Sufianimafoto, Mzee Cuf, aliyewahi kushiriki katika
mchakato wa kumuondoa Nduli Idd Amin Dada katika Mipaka ya Tanzania,
mwaka 1978, anasema kuwa pamoja na kuwa mkakamavu kutokana na kuwahi
kuwa 'Mjeda' Afande wa Jeshi la JWTZ na kushiriki Vita ya Kagera lakini
bado anaamini hatua kubwa ya maisha yake imetokana na Kamera ambayo hadi
hii leo anaitumia kwa kupiga picha za Banyaa na kumwezesha kujipatia
kipato chake cha kila siku cha kuitunza familia yake pamoja na matumizi
ya kawaida yanayohitajika katika familia.

"Kamwe
sitaweza kuacha kamera hii na kurukia katika hizo zenu za Bongo Flava,
akimaanisha kamera za Digital, kwani naiamini sana kamera hii ya mknda
kuliko hata hizo zinazowarahisishia mambo,




Unajua
kamera hizo ni sawa na Gari la Auto ambalo hata mlemavu ama mtoto
anaweza kuendesha kwa maelekezo kidogo tu, lakini gari ya Manu hata awe
mtu mzima ni lazima aende shule ndiyo aweze kuliondoa gari" alisema Mzee
Cuf.

Kwa
mujibu wa Mzee Cuf mwenyewe, alishiriki katika Vita ya Kagera akiwa
katika Kikosi cha Kakunyu No, 824 kilichokuwa chini ya Captain Alenguya.


No comments: