Tuesday, December 6, 2011

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Na Mbunge Wa Kitope Zanzibar Atembelea Jimbo Lake

Makamu
Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akikabidhi Hati Ya
Usajili Wa Saccos Ya Uwezeshaji Kwa Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Kazi Bibi
Asha Abdulla




Mbunge
Wa Jimbo La Kitope Balozi Seif Ali Iddi Akipokea Msaada Wa Seti Tatu Za
Kompyuta Kutoka Kwa Rais Wa Jumuiya Ya Khoja Shia Ithna-Asheri Zanzibar
Nd. Mohd Raza.Kompyuta Hizo Zenye Thamani Ya Shilingi Milioni
8,000,000/- Ni Ahadi Iliyotolewa Na Rais Wa Shirikisho La Jumuiya Ya
Kimataifa Ya Khoja Shia Ithna-Sheri Dr. Ali Dinna Aliyoitoa Tarehe 30
Mei Mwaka Huu Wakati Wakitoa Msaada Wa Madeski Kwa Skuli Za Jimbo La
Kitope.


Mbunge
Wa Jimbo La Kitope Balozi Seif Ali Iddi Akikabidhi Seti Za Jezi Na
Mipira 46 Kwa Timu 23 Za Soka Zilizomo Ndani Ya Jimbo La Kitope. Vifaa
Hivyo Vya Michezo Hutolewa Na Mbunge Huyo Kila Mwaka Ili Kuimarisha
Michezo Jimboni Humo.



Mke
Wa Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
Akiwanasihi Wake Wa Waheshimiwa Kuwasaidia Waume Zao Majimbo. Mama Asha
Alisema Hayo Katika Hafla Fupi Ya Uzinduzi Wa Kikundi Cha Ushirika Cha
Hatubaguani Wote Ni Sawa Cha Jimbo La Kitope.


Makamu
Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akizindua Kikundi Cha
Ushirika Wa Ushoni Cha Hatubaguani Wote Ni Wetu Cha Jimbo La
Kitope. Kikundi Hicho Pia Kimepatiwa Msaada Wa Vyarahani 16 Pamoja Na
Baadhi Ya Vifaa Kwa Ajili Ya Kuendeleza Mafunzo Yao Ya Ushoni.


Makamu
Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akipokea Maandamano Ya
Vikundi Vya Ushirika Vya Saccos Katika Maadhimisho Ya Wiki Ya
Uwezeshaji Zanzibar. Sherehe Hizo Zimefanyika Makao Makuu Ya Wizara Ya
Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Na Ushirika.


Makamu
Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Akiwa Katika Picha Ya
Pamoja Na Viongozi Wa Wizara Ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Na
Ushirika Na Baadhi Ya Viongozi Wa Saccos Ya Uwezeshaji.Picha Zote na
Ofisi ya Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar
--
Mbunge
wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi amelipongeza Shirikisho la
Kimataifa la Jumuiya ya khoja Shia ithna-asheri kwa juhudi zake za
kusaidia Maendeleo ya Elimu Hapa Zanzibar.
Balozi
Seif alitoa pongezi hizo baada ya Kukabidhiwa Seti tatu za Kompyuta
kutoka kwa Rais wa Shirikisho hilo Duniani Dr. Ali Dinna.
Rais
wa Jumuiya ya Koha Shia Ithna-sheri hapa Zanzibar Nd. Mohd Raza
amekabidhi msaada huo kwa Niaba ya Rais wa Shirikisho hilo hafla
iliyofanyika katika Skuli ya Kitope.
Balozi
Seif ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Maendeleo
makubwa yamepatikana ndani ya Jimbo la Kitope kutokana na kupata nguvu
za Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri.
Aliwaomba
wananchi wa Majimbo mengine kuhakikisha wanachagua Viongozi wazuri
watakaowaleteta maendeleo ya haraka katika Majimbo yao bila ya kuangalia
ujomba au rafiki.
Mapema
Rais wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna-sheri Zanzibar Nd. Mohd Raza
alisema Taasisi yao itaendelea kusaidia huduma za Kijamii, Elimu na
Uchumi ili kuona ukali wa maisha unapungua miongoni mwa Wananchi.
Kompyuta
hizo zenye thamani ya shilingi milioni nane ni utekelezaji wa ahadi ya
Uongizi wa Shirikisho hilo waliyoitowa tarehe 30 Mei mwaka huu wakati
wakikabidhi msaada wa madeski katika skuli zilizomo ndani ya Jimbo la
Kitope.
Wakati
huo huo Balozi seif alizindua Kikundi cha Ushirika cha Ushonaji
kiitwacho hatubaguani wote ni wetu cha jimbo la Kitope kinachoendelea
kupata mafunzo katika ofisi ya jimbo hilo hapo kinduni.
Balozi
Seif pia alikabidhi msaada wa vyarahani, mota pamoja na Vifaa mbali
mbali vya kujifundishia vikiwa na thamani ya jumla ya shilingi Milioni
2,325,000/-.
Akitoa
nasaha zake katika Hafla hiyo Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama
Asha Suleiman Iddi amewaomba Wake wa waheshimiwa kuwasaidia Waume zao
katika kufanya ziara za kujua matatizo yanayowakabili Wananchi.
Mama
Asha Alisema utaratibu huo utasaidia kuibua matatizo ya msingi na
kuleta upendo katika kuharakisha maendeleo ya pamoja kati ya Viongozi na
wanaowaongoza.

Kikundi
cha ushirika cha ushoni cha hatubaguani wote ni wetu chenye wanachama
45 kimelenga kutoa mafunzo kwa wnanchi wake kwa nia ya kusambaza ajira
miongoni mwa wanawake ambao ndio walezi wa




Familia popote pale.







Othman Khamis Ame





Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar





4/12/2011.

No comments: