Sunday, December 11, 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HAFLA YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KIISLAM WA 1433

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba wakati wa halfa ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tanzania Tawi la Dar es Salaam. Hafla hiyo ilifanyika leo Desemba 11, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee jijini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alilopata nalo ajali Bw. Arif Yusuph, eneo la Mji wa Fiche Kilometa 100 kabla ya kufika Adis Ababa , wakati akitoka Kuhij Makha baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya Hice iliyokuwa imebebea Jeneza ikisafirisha msiba, katika ajali hiyo watu wote walisalimika na kurejea nyumbani. Makamu wa Rais alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Desemba 12.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Msaafu kutoka kwa, Sheikh Ahmed Mohamed Lbadry, baada ya kumaliza hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la dare s Salaam na kufanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo Desemba 12.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakati akiondoka kwenye Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam, leo Desemba 12, baada ya kumaliza shughuli ya hafla ya kuukaribisha mwaka mpya wa Kiislam iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiqaama Tawi la Dar es Salaam.
Waumini wakiomba dua baada ya kumalizika hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama, baada ya kumalizilika kwa half hiyo leo Desemba 12.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments: