Saturday, December 3, 2011

MBUNGE WA IRAMBA MAGHARIBI MKOANI SINGIDA AKUMBANA NA ADHA YA BARABARA MBOVU.


Katibu wa uchumi na fedha CCM Taifa na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mh. Mwigullu Lameck Nchemba (mwenye skafu),akisaidia kulinasua gari lake lililokuwa limekwama kwenye mto Ndurumo kata ya Kidaru.




Mbunge Mwigullu alilazimika kubadilisha nguo ili kuendelea na kazi ya kulinasua gari lake lililokwama kwenye mto Ndurumo.




Baada ya kazi kuwa ngumu,mbunge Mwigullu alilazimika kutafakari mbinu zaidi la kulinasua gari lake lililokwama kwenye mto Ndurumo.




Mbunge Mwigullu,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya ubovu wa miundombinu ya barabara kati jimbo lake.




Msaidizi wa mbuge huyo akiwa kwenye harakati ya kunausa gari la bosi wake.(Picha zote na Nathaniel Limu).


Na.Nathaniel Limu.


Katibu wa uchumi na fedha wa CCM taifa na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mwigullu Lameck Nchemba, ameonja adha ya barabara mbovu baada ya gari lake kukwama mtoni na kulazimika kulinasua kwa zaidi ya saa nne.


Katibu huyo ambaye alikuwa amefuatana na Kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Frank Kisanga, walikuwa kwenye ziara ya siku moja ya kukagua miundombinu ya barabara katika jimbo la Iramba Magharibi.


Barabara hizo ni pamoja na ile iliyopandishwa hadhi na kuwa ya mkoa inayoanzia Kiomboi mjini – Kisiriri – Kidaru.


Gari hilo la Katibu Mwigullu lilikwama kwenye mto Ndurumo katika kijiji cha Ndurumo kata ya Kidaru wilayani Iramba.


Gari hilo aina ya GX 8 lilinasuliwa na wapiga kura wa Mwigullu na wananchi wa kijiji cha Ndurumo na hivyo kuendelea na ukaguzi wa barabara ya Kidaru – Doromoni hadi Shelui.


Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge huyo amewataka makandarasi kujenga/kukarabati barabara zinazofanana na thamani ya fedha zinazotumika na si vinginevyo ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.


Amesema miundombinu ya barabara ni muhimu mno kwa maendeleo ya wananchi hivyo ni lazima zijengwe au zikarabatiwe kwa ubora unaoainishwa kwenye mikataba husika.


Mwigullu amesema kuanzia sasa hatakubaliana na makandarasi wanaopewa kazi ya kukarabati au kujenga barabara halafu wanafanya kazi hiyo chini ya kiwango.


Katika hatua nyingine Mwigullu amesema shilingi milioni 89.5 zilizotengwa kwa kazi ya ukarabati wa barabara ya Kiomboi – Kisiriri – Kidaru hazitoshelezi.


Ametumia fursa hiyo kuiomba serikali iangalie upya uwezekano wa kuiongezea fedha barabara hiyo ambayo inapitika kwa taabu karibu kipindi chote cha mwaka.


Kwa upande wake kaimu meneja wa TANROADS mkoa wa Singid Mhandisi Kisanga amesema tayari tenda ya kukarabati barabara ya Kiomboi – Kisiriri – Kidaru imeishatangazwa na makandarasi wamekwisha omba ila kinachosubiriwa ni kuzifungua tu ili kazi iweze kuanza.
Habari kwa Hisani ya Mo-Blog

No comments: