Sunday, December 18, 2011

Mjengwablog Young Leaders Award-2011: Matokeo Rasmi Haya Hapa...

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Kifurahia Jambo na Mbunge wa Kawe-Chadema Mheshimiwa Halima Mdee Nje ya Viwanja Vya Bunge Mjini Dodoma Hivi karibuni
Mbunge wa Arusha Mjini-Chadema Mheshimiwa Godbless Lema akiongea na Waandishi wa Habari kwenye moja ya Mikutano yake
--
Ndugu zangu,



Kufuatia mchakato wa majuma kadhaa wa kuwapata wabunge bora vijana kwa mwaka 2011, hatimaye mchakato husika umemalizika rasmi jana asubuhi www.mjengwablog.com inawashukuru wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.



Na shukrani za kipekee kwa wale waliochukua muda wao kupiga kura.
Mchakato wa kwanza ulikuwa ni wa kundi la wanawake. Jumla ya kura 514 zilipigwa. Matokeo ya washindi watatu wa kwanza ni kama ifuatavyo:
1.

1.Halima Mdee- kura 395 ( 72%)
2. 2. Regia Mtema-kura 32 ( 5%)
3. 3 Esther Bulaya- kura 21 ( 3%)


Kwa upande wa wanaume jumla ya kura 8576 zilipigwa. Matokeo kwa washindi watatu wa mwanzo ni kama ifuatavyo:
1.

1.Godbless Lema - Kura 4310( 50%)
2. 2. Zitto Kabwe - Kura 3074 ( 35%)
3. 3. John Mnyika - Kura 776 ( 9%)
Kinachofuata:



Utaratibu wa kukabidhi tuzo na zawadi kwa washindi unaandaliwa. Kama watatokea wenye kutuunga mkono na kushirikiana nasi, basi, inatarajiwa tuzo hizo zitatolewa katika tarehe itakayopangwa mwezi Februari mwakani. Taratibu zinaandaliwa kuwezesha tuzo hizo kutolewa sambamba na kufanyika mjadala wa vijana juu ya masuala muhimu ya kitaifa yenye kuvuka mipaka ya vyama.



Mjadala utakaowashirikisha washindi, walioshiriki mchakato katika hatua ya fainali, wanaharakati vijana na wanasiasa vijana waliokwisha pendekezwa hadi sasa kushiriki mchakato wa mwakani, marais wa jumuiya za wanafunzi wa vyuo vikuu, wanahabari, waandishi wachambuzi wa makala za magazetini na wageni waalikwa. Kutakuwa na mada fupi zitakazowasilishwa na washindi wa kwanza wa tuzo. Mada zitakazowasilishwa kwa dakika kumi na tano kwa kila mshindi wa kwanza toka kwenye kundi lake. Muda huo utaruhusu washindi wa tuzo kujibu maswali kadhaa toka kwa washiriki na pia kuruhusu mjadala mpana.



Madhumuni ya tuzo:



Kuhamasisha ushiriki wa vijana kwenye masuala ya uongozi wa siasa. Hivyo basi, kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana wa KiTanzania katika kushiriki kujenga na kuimarisha misingi ya kidemokrasia. Kwamba vijana washiriki kwenye kujenga mustakabali wa nchi yetu bila kujali tofauti zao za kiitikadi, kidini, kikabila, kimaeneo na hata rangi.



Mipango ya baadae:

-Kuifanya tuzo hii ya ‘ Mjengwablog Young Leaders Award’ kuwa ni ya kila mwaka.
-Mwakani itashirikisha pia kundi la wanaharakati vijana na wanasiasa vijana wanaochipukia.
- Mjengwablog itawashirikisha wadau wengine katika kushiriki na kuboresha mchakato huu ili kufanikisha madhumuni ya kuanzishwa kwa tuzo hii ambayo bila shaka ni yenye tija kwa taifa.



Mwisho kabisa:



Kama mratibu a mchakato, nawashukuru wote waliochangia kwa njia moja moja au nyingine. Nawashukuru sana wale wote walioona haraka umuhimu wa jambo hili na walionitia moyo tangu waliposoma habari za mchakato huu kwa mara ya kwanza.



Pia nawashukuru sana wale wote waliochachamaa na kuushutumu mchakato huu tangu siku ya kwanza. Ndipo hapo nilipoona kuwa jambo hili ni muhimu sana. Na hakika kulikuwa na shutuma nyingi njema zilizosaidia na zitakazosaida kuboresha mchakato huu kwa siku zijazo.



Wenu,



Maggid Mjengwa,
Iringa.
Jumapili, Desemba 18, 2011
www.mjengwa.blogspot.com

0788 111 765, 0754 678 252



No comments: