Wednesday, December 7, 2011

Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru katika uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akizungumza katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru katika uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza, sherehe ambazo kimkoa zitafanyika wilayani Korogwe Desemba 9. Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza umuhimu wa wananchi mkoani Tanga katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru kubadili mtazamo wa kutumia fursa na rasilimali zilizopo mkoani humo kujiletea maendeleo. Alisema mkoa huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa wananchi watumie ardhi yenye rutuba kulima na kujitosheleza kwa chakula ikiwemo kuongeza ushindani katika mazao ya biashara. Wengine kaika picha ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Bw. Methew Nasei (Kushoto), Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Bw. Peter Jambele na Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bw. Benedict Ole Kuyan.
baadhi ya viongozi waliofuatana na Mkuu wa mkoa wa Tanga, wakisikiliza hotuba mbalimbali za kiongozi huyo wakiwemo waasisi wa Uhuru wa Tanganyika. kutoka kushoto ni Mbunge wa Muheza CCM Bw. Herbert Mntangi, Msaidizi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga Bw. Joseph Sura, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Bw. Amir Kiroboto na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Tem Goliati.Picha na Mdau Mashaka Mhando, Mzee wa Bonde.
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog

No comments: