Thursday, December 29, 2011

MSANII MOS P. AKONGA NYOYO ZA MASHABIKI WAKE KIJIWENI KWA MUSSA SHOE SHINE

Hapa mashabiki wake wakimuangalia wakati alipokuwa akitoa burudani ya muziki wake kama anavyoonekana katika picha hii.
Jana katika pitapita yangu nilikutana na kijana Amos Pauson aka (Mos P.) kutoka kijiji cha Ifumbo Wilayani Chunya mkoani Mbeya ambaye ni msanii wa muziki wa asili, msanii huyu alikuwa akitoa burudani yake katika kijiwe kimoja maarufu mtaa wa Samora karibu na Idara ya Habari Maelezo au kama kinavyojulikana kwa (Mussa Shoe Shine), kijiwe hiki hutembelewa na wajanja wengi wa mjini na watu maarufu kwani Mussa ni mg'arisha viatu wa siku nyingi hapo, hivyo anafahamika sana na watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu.

Jana kijana huyu alikuwa akitoa burudani katika kijiwe hicho kilichokuwa kimesheheni watu wengi akiwemo mpiga picha wa siku nyingi Shabaan Madanga aliyewahi kuwa mpiga picha katika magazeti ya serikali.

Jambo kubwa nililoliona hapo ilikuwa ni furaha ya watu waliokuwepo katika kijiwe hicho kutokana na burudani ya muziki iliyokuwa ikitolewa na kijana Mos P. wakati akipiga gitaa lake la lililotengenezwa kwa mti, kopo na ngozi ya ngombe, huku likiwa limefungwa nyuzi tatu tu zinazotoa ladha murua ya muziki wake mara apigapo na kuimba.

Kijana Mos P. anasema anayo albam inayoitwa Tamaa yangu yenye nyimbo kadhaa ambazo nini Tamaa yangu yenyewe, Sali Kumwanya ikiwa na maanna twende mbinguni ,Roda,Vumilia,Wonti Upena yaani wote umasikini, Ukimwi nooma, Nasukwa Khuhaya yaani nimekumbuka nyumbani na anaongeza kwamba bado anazo nyimbo nyingi sana ambazo hajarekodi.

Mos P ameongeza kwamba albam hii amerekodi katika studio za Mambo jambo kwa Benjamin huko Mbezi, lakini pia amesema kwa sasa anafanya kazi ya kupiga muziki jijini Dar es salaam kwa kupata kiasi kidogo cha fedha zinazotolewa na mashabiki wake mara apigapo muziki wake maeneo mbalimbali akikusanya fedha kwa ajili ya kurekodi video ya nyimbo hizo.


No comments: