Thursday, December 29, 2011

TRA kuanza kutoza VAT Januari 1, 2012 kwa wageni

Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani, Christine Shekidele (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kususiana na Ongezeko la Thamani (VAT) na faida zake kwa Taifa
Mkurugenzi wa Fedha TRA, Saleh B. Mashoro akitoa maelezo juu ya mpango wa mamlaka hiyo wa kukusanya Ongezeko la Thamani kwa wageni watakaosafirisha bidhaa za ndani kupeleka nje ya nchi

Na Emmanuel Kimweri wa Fullshangwe - Dar es salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuanzia tarehe 1, Januari 2012 inaanza rasmi kushughulikia marejesho ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa wasafiri wakigeni wanaondoka kwenda nchi za nje kwa mujibu wa sheria ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha TRA, Saleh B. Mashoro, alisema utaratibu huu wa kukusanya VAT umekuwa ukitumika na nchi mbalimbali duniani kutokana na ukweli kuwa VAT ni kodi inayotokana na matumizi.
“TRA imevuka malengo ya mwaka kwa kukusanya shilingi trillion mbili, bilioni nne na sabini na na tano (Trilioni 2.475 bilioni) malengo ni kukusanya trilioni mbili, bilioni nne na sabini na nne (Trilioni 2.474) hii ni kuanzia Novemba mwaka jana hadi sasa”, alisema Mashoro.
Alisema VAT itakayotozwa kwa wageni pindi watakapo safirisha bidhaa kutoa ndani ya nchi kupeleka nje ya nchi kwa kuthibitishwa na maasira wa TRA kuwa bidhaa hiyo haijatumika.
“Gharama ya marejesho ni asilimia tano (5%), ya kiasi cha marejesho na gharama hii italipwa na muombaji wa marejesho’ alisema
Aliendelea kusema katika kuhakikisha zoezi lina kwenda vizuri tumeweka Wakala wa Marejesho ambao ni Benki ya TWIGA BANCORP ambayo itakuwa na ofisi zake katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam (DIA) na Kilimanjaro (KIA)
Aidha, Mamlaka inawataka wale wote ambao wanaostahili kudai marejesho sanjari na umma wote kwa ujumla wake kushirikiana na TRA ili kutoa huduma bora yenye ufanisi wa hali ya juu kwa kuzingati sheria zinazohusika.

No comments: