Tuesday, December 6, 2011

SPIKA WA BUNGE ANNE MAKINDA AZINDUA RIPOTI YA DUNIA YA UMOJA WA MATAIFA KUHUSU HAKI,IDADI YA WATU NA UJANA TANZANIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akimpongeza kijana Mohamed Kessy kutoka Mbeya mara baada ya kijana huyo kuwasilisha matamko mbalimbali ya watoto yakiwemo uboreshaji wa elimu,utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa jamii, elimu ya maambukizi ya VVU na Ukimwi, Masuala ya ulinzi na ukatili dhidi ya watoto pamoja na sheria zinazolinda na kutetea haki za watoto leo jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge Anne Makinda akimpongeza msaanii wa muziki wa kizazi kipya Bakari Hassani maarufu kwa jina la BECCA mara baada ya kuimba wimbo wake wa Natumaini uliokua na ujumbe maalum kwa vijana kujiepusha na matumizi ya Pombe na Bangi leo.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiongea vijana na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki za watoto, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akitoa ujumbe wa umoja wa mataifa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo ongezeko la idadi ya watu,masual ya wanawake na watoto leo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi mkazi wa UNICEF nchini Tanzania Bi. Dorothy Rozga akitoa ujumbe maalum wa shirika hilo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana leo jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akizindua ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki za watoto nchini, idadi ya watu na masuala ya vijana akiwa ameungana na baadhi ya vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini leo jijini Dar es salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya watu, Haki za watoto na masuala ya wanawake na watoto leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya vijana waliohudhuria uzinduzi wa ripoti ripoti ya dunia ya umoja wa mataifa kuhusu Haki, idadi ya watu na masuala ya vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ya spika wa Bunge Anne Makinda ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

No comments: