Wednesday, December 7, 2011

TAASISI MBALI MBALI ZACHANGIA MFUKO WA HASSAN MAAJAR TRUST DAR


Balozi Mwanaidi Maajar ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi Hassan Maajar Trustakizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua madawati katika shule mbalimbali nchini iliyoandaliwa na taasisi hiyo, hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu, na imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu wa serikali pamoja na baadhi ya mawaziri na wakuu wa makampuni mbalimbali jijini Dar es salaam. Kauli mbiu ya hafla hiyo ni A Desk For Every Child.

Mkurungenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu Kyando kulia akiteta jambo na Mbunge wa Musoma vijijini Mh. Nimrod Mkono katika hafla hiyo.

Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo usiku huu.

Mkurugenzi wa Radio One Deo Rweyunga katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho cha Radio.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa akishiriki katika hafla hiyo pamoja na wageni wengine waalikwa kushoto ni maiwaifu wake Anna Slaa.

Kutoka kulia ni Joseph Tadayo, Joachim Tenga na Jeff Tenga wakiwa katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru kulia akiwa ni mmoja wa wageni waliohudhuria katika hafla hiyo , kushoto ni Mwanamitindo Flaviana Matata akiwa na rafiki yake katikati,Yvonne Mashuda.

Waziri Mkuu mstaafu Fredirick Sumaye akisalimiana na Balozi Mawaidi Maajar wakati Mh. Sumaye alipowasili ukumbini hapo, kulia ni Mama Esther Sumaye.

Waziri Mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba kulia akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serenget SBL Mzee Mark Bomani.
Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika hafla hiyo usiku huu.

Kundi la muziki la THT likitumbuiza katika hafla hiyo inayofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Hawa ndiyo viongozi wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipokuwa wakitambulishwa na Balozi Mwanaidi Maajar.
(picha kwa hisani ya FULL SHANGWE)

No comments: