Monday, December 26, 2011

Waraka wa Pili wa Mbunge kwa Wananchi wa Jimbo la Ubungo


Uhuru na Kazi:
Nimekuja
kuwatembelea kuona hali halisi ya uharibifu wa makazi yenu, mali zenu
na miundombinu yetu kutokana na maafa ya maafuriko katika mitaa hii ya
kata ya mabibo. Kuanzia maafa yatokee tarehe 20 Disemba mpaka tarehe 24
Disemba nimekuwa pamoja na wananchi wenzangu wa jimbo la Ubungo bega kwa
bega katika jitihada za uokoaji na utoaji wa huduma za kijamii katika
maeneo mbalimbali mathalani Msewe, Ubungo, Kisiwani, Kibo, Mburahati,
Sinza D, Sinza E, Uzuri, Manzese Chakula Bora, Mburahati Kisiwani,
Msigani, Mbezi Kibanda cha Mkaa, Kimara B. Na pia, nimeenda kutoa
misaada kwa majimbo jirani ya Kinondoni (Magomeni Sunna na Kigogo), Kawe
(Msasani Bonde la Mpunga na Bunju) na Ilala (Mchikichini). Kutokufika
Mabibo, katika hizo siku chache, kunadhihirisha ukubwa wa maafa yenyewe
na ilikuwa vigumu kuwepo mahali pote wakati wote. Hata hivyo, katika
wakati huo wote nilikuwa na mawasiliano na wananchi na viongozi
kuhakikisha kwamba mamlaka zinazohusika na uokoaji zinafika katika
maeneo haya. Nawashukuru wote mliotoa ushirikiano wakati wa uokoaji na
nawashukuru pia mliotoa msaada wa hali na mali kwa majirani zenu katika
kipindi hiki kigumu.

Nimekuja kwenu leo katika sikukuu ya
kufungua zawadi (boxing day) kutoa michango yangu ya chakula na mavazi
kwa waathirika wa maafa wasio na uwezo; hata hivyo zawadi yangu kubwa
kwenu leo; sio vitu hivi tulivyotoa, ni waraka ninaoutoa kwenu wananchi
wenzangu wa jimbo la Ubungo. Waraka huu naamini utakuwa ‘chakula’ cha
fikra kwenu leo na kesho kwa ajili ya mabadiliko katika maisha yetu na
taifa letu.

Katika waraka wangu wa kwanza kwenu niliwapa mrejesho
kuhusu uwakilishi wa Mbunge katika mkutano wa pili wa Bunge.
Nawaandikia waraka huu “Uhuru na Mabadiliko” katika mwaka 2011 wa
kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo sasa inaitwa
Tanzania bara.

Lengo la waraka huu ni kuungana nanyi katika mwaka
huu kutafakari kila mmoja wetu kuhusu taifa letu lilipotoka, lilipo na
tunapotaka liende katika kipindi cha miaka 50 toka Uhuru na kutumia
fursa hiyo pia kutafakari kuhusu jimbo letu katika kipindi cha mwaka
mmoja toka uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na kuwatakia heri ya mwaka mpya
wa 2012.

Waraka huu wote, isipokuwa aya ya kwanza na aya hii ya
tatu, niliuandika tarehe 9 Disemba 2011; hata hivyo sikuutoa siku hiyo
kutokana na ‘macho na masikio’ ya wengi kuelekezwa katika ‘sherehe’ za
siku hiyo pamoja na matarajio kuhusu hotuba ya Mkuu wa Nchi kugusa
masuala mapana kuhusu mwelekeo wa taifa. Nimeona niutoe waraka huu
katika kipindi cha kuelekea mwisho wa mwaka, na ni wakati muafaka wa
kutafakari zaidi baada ya ‘sherehe’ kwa kuwa mpaka sasa Rais Jakaya
Kikwete hajatoa hotuba nyingine ndefu kama alivyoahidi tarehe 9 Disemba
na pia taifa linamaliza majonzi yaliyotokana na maafuriko yaliyoleta
maafa katika mkoa wa Dar es salaam


Kwa kuendelea Kuisoma <<< BOFYA HAPA >>>

No comments: