Thursday, December 22, 2011

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli Ashuhudia Utiaji Saini Wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es salaam

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akionyesha baadhi ya ramani yenye michoro ya barabara za juu (Flying- Over) zitakazojengwa jijini Dar es Salaam. mbele ya waandishi wa habari na Wadau wa sekta ua Ujenzi leo,wakati ya hafla ya uwekaji wa sahihi ya Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mfumo wa Usafiri haraka wa mabasi jijini Dar es salaam.awamu ya kwanza,Kandarasi ya kwanza (barabara),utakapo kamilika ujenzi wa barabara hizo itasaidia kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salam,ambapo ndio lengo kubwa la serikali.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL Gmb ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakibadilishana hati za mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,.Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS )Mhandisi Patrick Mfugale (kushoto) pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Mkandarasi M/S STRABAG INTERNATIONAL GmbH ya Ujerumani Heribert Schippers (kulia) wakitiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mfumo wa Usafiri Haraka wa Mabasi jijini Dar es Salaam Awamu ya kwanza, Kandarasi wa Kwanza (Barabara) Nov.22.2011 katika makao Makuu ya Wizara ya Ujenzi,. Mradi huo wa Ujenzi unafadhiliwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia ambapo mradi mzima wa kazi utagaharimu shilingi 240.9 Bilioni. Ujenzi wa awamu ya kwanza unahusisha ujenzi wa barabara unaofikia kilometa20.9 katika barabara ya Morogoro(kutoka Kimara hadi Kivukoni (Feri), barabara ya Kawawa (kutoka) Magomeni hadi Morocco ) na barabara ya Msimbazi (kutoka Fire hadi makutano ya Nyerere -KAMATA). Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli , Viongozi wa TAMISEMI, Wizara ya Fedha na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi.
Picha na Mwanakombo Juma-MAELEZONo comments: