Wednesday, January 11, 2012

Dk. Ali Mohamed Shein asamehe wafungwa 22

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa wafungwa (Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo) 22 ikiwa ni miongoni mwa sherehe za kutimiza miaka 48 ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ikulu Zanzibar zimeeleza kuwa kwa mujibu wa uwezo aliopewa kisheria chini ya kifungu namba 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein ametoa msamaha huo kwa wafungwa (Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo) 22.
Msamaha huo ambao hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi huwahusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au wenye vifungo vidogo vidogo na kuonesha nidhamu nzuri chuoni.

Wafungwa (Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo) wenye makosa kama vile wizi wa kutumia nguvu, wizi wa mali ya serikali, makosa ya kudhalilisha wanawake na watoto, makosa ya dawa za kulevya na wenye makosa mengi ya zamani kwa kawaida huwa hawapewi msamaha.

No comments: