Wednesday, January 25, 2012

GARI YAWAKA MOTO JENGO LA AMANI PLACE LEO


Asalam Aleykum Ustadh Issa,

Pole na baridi linalokupiga huko Davos, Uswisi..

Hakuna tunachokunyima Dar zaidi ya joto tu..Nadhani joto hili la hapa kwetu ndo limesababisha mpaka gari hili kuungua...

Hii imetokea just now...hapa kwenye parking za jengo la Amani Place. Upande wa nyumba karibu na Citibank.

Zimamoto walifanikiwa kuisukuma na kuitoa eneo la parking ili isisababishe madhara kwa magari mingine..lakini almanusura wasababishe ajali nyingine baada ya kuiachia gari hiyo kwenda yenyewe hadi upande wa pili wa barabara na kumkosakosa jamaa aliyekuwa amepaki pikipiki akiangalia uokoaji wa gari hilo.

Chanzo cha gari hilo aina ya Toyota Surf kushika moto halijafahamika hadi sasa..na mwenye mali yake hajaonekana wala kujitambulisha.

Injini ya gari imeungua yote.

Mdau wa Globu ya Jamii alieshuhudia Tukio
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI BLOG

No comments: