Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unafuraha kuwataarifu kuwa kuanzia Jumatano ijayo Januari 18, 2012 huduma za safari za treni za abiria kutoka Dar kwenda Kigoma zitaanza na kwamba wananchi wanaotaka kusafiri na treni zake za wafike katika stesheni husika kukata tiketi za safari kuanzia kesho Jumatatu asubuhi Januari 16, 2012.
Kuanza tena huduma hiyo kumetokana na kukamilika kazi ya ukarabati hapo Januari 12, 2012 ambayo imewezesha treni za mizigo zipatazo 10 kutoka na kwenda bara kupita eneo la Godegode mkoani Dodoma kuanzia siku hiyo.
Hata hivyo mafundi wa TRL bado wanaendelea na kazi ya kuimarisha tuta la reli katika maeneo mawili korofi eneo la Stesheni ya Godegode ambayo hukumbwa na mafuriko na kusababisha reli kuhabirika.
Huduma za treni zilisimamishwa Januari 07, 2012 baada ya kutokea uharibifu mkubwa katika eneo la stesheni za Godegode kufuatia mafuriko yaliyokumba eneo kutokana na mvua kubwa ziliznyoesha katika mikoa ya Mororogro, Iringa na Dodoma.
TRL ilikuwa ikipoteza takriban mapato ya Shilingi milioni 81.3 kwa kila siku kwa kufuta safari za treni za mizigo na wastani wa shilingi milioni 59 kwa wiki kutokana na kufuta safari 4 za treni za abiria.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi K.A.M. Kisamfu.
Imesainiwa na :
MIDLADJY MAEZ
MENEJA UHUSIANO
MAKAO MAKUU YA TRL
DAR ES SALAAM
JANUARI 15, 2012
No comments:
Post a Comment