Sunday, January 15, 2012

UP DATES ya MSIBA WA MHESHIMIWA REGIA ESTELATUS MTEMA

Katika taarifa yetu ya jana, tulieleza kwamba tutaendelea kutoa taarifa hatua kwa hatua, kuhusu msiba na maziko ya Marehemu Regia Estelatus Mtema aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira.

Kwa sasa tunaomba kuwataarifu kwamba kufuatia mashauriano baina ya familia, Ofisi ya Bunge na chama; heshima za mwisho kwa marehemu zitatolewa siku ya Jumanne, Januari 17, 2012. Baada ya kuagwa, marehemu atasafirishwa mpaka Ifakara ambapo maziko yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Januari 18, 2012.

CHADEMA tunaendelea kujumuika na familia ya Regia Mtema, bunge na wapenda demokrasia na maendeleo wote nyumbani kwa baba wa marehemu, eneo la Tabata Chang'ombe.

Marehemu Regia Mtema ni nyota iliyotoweka mapema lakini kumbukumbu yake itaendelea kuwepo kwa chama na kwa taifa. Apumzike kwa amani.

Imetolewa leo Januari 15, 2012

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

No comments: