Friday, January 20, 2012

Kesi Ya Mbunge Wa CUF Hamad Rashid Na Chama Chake Yahamia Mahakama Kuu

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF),Julius Mtatiro, akiwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakitoka Mahakama Kuu, katika kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho, waliofukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi, wakiongozwa na Mbunge wa Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, wakidai warejeshewe uanachama wao kwa kuwa wamefukuzwa isivyo halali na Baraza hilo na pia kukiukwa amri ya mahakama ya kulitaka baraza hilo, kutowajadili wala kuwafukuza unachama.
Mbunge wa Wawi kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akitoka katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam jana, baada ya kuahirishwa kwa maombi ya kutaka kujua hatima ya zuio la mahakama lililopuuzwa na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), katika kikao cha kuwafukuza uanachama. Kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Micheweni, kisiwani humo, Shoka Khamis Shoka na kushoto ni aliyekuwa mgombea wa chama hicho, Jimbo la Segerea, Kimangale Mussa.
Picha na Kassim MbaroukNo comments: