Wednesday, January 18, 2012

MAELFU WAJITOKEZA MAPOKEZI YA MH.REGIA MTEMA IFAKARA









Maelfu
ya wananchi wa mji wa Ifakara wakiwa barabarani ambako walizuia
ambulance iliyobeba mwili wa marehemu.Kwa mujibu wa wenyeji, haijawahi
kushuhudiwa mapokezi kama haya katika msiba wowote ule katika historia
ya mji huu.Mwenyekiti wa CHADEMA taifa alilazimika kuwaomba vijana
kutulia kwani walikuwa wamejawa na jazba na taharuki.Baada ya mwili
kuingizwa katika nyumba ya familia kwa muda, ulihamishiwa hospitali hadi
baadaye utakapotolewa kwa ratiba nyingine.Msafara kutokea Dar es salaam
uliwasili Ifakara saa 4 usiku na maandamano yaliuchelewesha kufika
nyumbani kwa marehemu.wageni kutoka dar es salaam walifika ndani saa 5
usiku.Msafara kutoka Dar es salaam ulikuwa na magari yapatayo 60,ambayo
mwandishi wa habari hii aliweza mwenyewe kuhesabu.Tutaendelea
kuwahabarisha kutokea Ifakara.



Mdau wa Mjengwablog,Ifakara

1 comment:

Suchilila said...

R.I.P Mh Regia Mtema, tutakukumbuka daima kwa uchapakazi wako. Tuliobaki tuendeleze mazuri yake daima.