Tuesday, January 17, 2012

Rais kikwete azindua madaraja makubwa mawili morogoro vijijini, aweka jiwe la msingi la soko, ahutubia katika mvua kubwa.


Rais Kikwete akiongea na baadhi ya wananchi baada ya kuzindua daraja la mto Mtombozi tarafa ya Matombo wilaya ya Morogoro mjini leo January 17, 2012
Rais Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera (shoto) akivuka daraja jipya la Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, Morogoro Vijijini baada ya kulizindua
Rais Kikwete akielekea jukwaani kuhutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa soko la kijiji cha Mtamba, Morogoro vijij
Rais Kikwete na ujumbe wake na wenyeji wakipita juu ya daraja jipya la Mtombozi, Matombo, Morogoro vijijini alilozindua leo. Rais Jakaya Kikwete leo ametembelea Morogoro vijijini na kuzindua madaraja mawili makubwa katika mto Mtombozi, Matombo, na mto Magogoni katika barabara ya Kiganila-Mvuha, pia ameweka jiwe la msingi la soko la kijiji cha Mtamba na kukagua ujenzi wa barabara sehemu ya Kisaki, Msalabani.

No comments: