Monday, January 16, 2012

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KICHINA DAR ES SALAAM

Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya waKichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini(CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar esSalaam jana jioni Januari 15.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwaBalozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa naCity Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafurikoyaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana,ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichinazilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari15.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwaBalozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa naChama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili yakusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaammwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe zakuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vyaMnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng ,wakati alipohudhuria sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina,zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT),zilizofanyika jana jioni Januari 15, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmojajijini Dar es Salaam.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiagana na baadhi ya wasanii wa Kichina waliokuwa wakitoa burudanijukwaani wakati wa sherehe hizo, wakati akijiandaa kuondoka katikaViwanja hivyo.
MakamuWa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akiongoza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, wakatiakiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioniJanuari 15, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina,sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini(CBCT)
Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais

No comments: