Tuesday, January 31, 2012

MH. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AKANUSHA KUBARIKI ONGEZEKO LA POSHO ZA WABUNGE

Dar Es Salaam,Tanzania, United Republic of

Rais Jakaya Kikwete leo amekanusha taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini Tanzania kuwa amebariki ongezeko la posho za wabunge na kufikia shilingi 330,000 kwa siku

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Maelekezo ya Rais Kikwete kuhusu suala hilo hakuna mahali ambako Rais Kikwete amebariki posho hizo

Taarifa hiyo imesema kuwa Rais Kikwete anakubali haja ya kuangalia upya posho kwa Wabunge lakini amewataka wabunge kutumia hekima na busara katika kulitafakari suala hilo

Pia amewataka Wabunge kutumia Kikao cha sasa cha Bunge kulizungumza upya suala hilo

Jumanne ya wiki hii gazeti la mwananchi limeripoti kuwa Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku na kufanya mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.


No comments: