Tuesday, January 24, 2012

RAISI JAKAYA KIKWETE NA VIONGOZI WENGINE WA SEREKALI WASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU JEREMIA SUMARI...!!!






Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha. Nyuma ni Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda na Spika mtaafu wa Bunge Mhe. Pius Msekwa






Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari kabla ya kwenda kuzika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha






Waombolezaji wakitremsha kaburini mwili wa aliyekuwa mbunge wa Arumeru Mashariki Jaeremiah Sumari katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Akeri, Arumemru, Januari 23, 2012.






Wananchi wa Arumeru kwa kushirikiana na vijana wa UVCCM taifa wakiufukia mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru mashariki Mhe. Jeremia Sumari wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha Leo






Miriam Sumari, mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jeremiah Sumari akweka shada la maua kwenye kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika Akeri, Arumeru, Januari 23, 2012.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha






Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe. Jeremia Sumari baada ya mazishi yaliyofanyika kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha






Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji mke wa Marehemu Mweshimiwa Jeremia Sumari, Bi. Miriam Sumari kabla ya mazishi ya marehumu sumari kijijini kwao Akheri, Mkoani Arusha






Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Marehemu Jeremiah Sumari katika mazishi ya mbunge huyo Akeri, Arumeru Januari 23, 2012.

(Picha na Owen Daudi na Ofisi ya Waziri Mkuu)





No comments: